in

Programu 4 Zinazoweza Kusaidia Kuroot Simu ya Android

Root simu yako ya Android kwa kutumia programu hizi

kuroot simu

Kwa wale ambao wanataka kujaribu kuroot simu zao makala hii itawasaidia kuweza kurahisisha kazi hiyo, kumbuka unapo root simu yako unapoteza haki yako ya kudai warranty pia kwa namna moja au nyingine unaweza kuharibu simu yako hivyo ni vyema kuwa makini unapotumia programu hizi na nakushauri usitumie programu hizi kama hujui unchofanya.

Nini Maana ya Kuroot

Basi kwa kusema hayo labda tuongelee kidogo kuhusu maana ya kuroot, Kuroot ni kitendo cha kuondoa kikomo cha uwezo wa simu za Android kwa kutumia programu maalum inayo julikana kama superSU. Programu hii inatoa uwezo wa baadhi ya programu ndani ya simu yako kuweza kufikia mafaili ya ndani ya mfumo wa uendeshaji wa Android ambayo mara nyingi huwa yamefichwa kwa ajili ya usalama wa kifaa chako.

Faida na Hasara za Kuroot Simu

Japokuwa kuroot simu kuna hasara kubwa kuliko faida lakini hebu tuangalie baadhi ya faida zinazopatikana unapo root simu yako ya Android. Moja kati ya faida kubwa ambayo unaweza kupata ni uwezo wa kubadilisha muonekano wa simu yako kwa namna mbalimbali. Kama wewe ni mbunifu wa programu au kama unasoma makala hii basi kwa namna moja ama nyingine lazima utakuwa unajua umuhimu wa kuroot simu yako. Kwa kuroot simu ya android unaweza kubadilisha ROM ya simu yako, pia unaweza ku-flash simu yako bila kuwa na kompyuta pamoja na faida nyingine nyingi kama kuongeza nguvu ya simu yako.

Apps za Kusaidia Kujibu Meseji WhatsApp (Bila Kushika Simu)

Kwa upande wa hasara, Kuroot simu yako kuna hasara nyingi zaidi hata hivyo moja ya hsara hizo ni pamoja na kuharibu simu yako(Briking), pia kunaweza kufanya simu yako iwe rahisi zaidi kudukuwa (Hack), pia kuna wakati programu za Google hazifanyi kazi vizuri kwenye simu za Android ambazo zimekuwa rooted, vile vile kuna wakati simu zilizo kuwa rooted zinapoteza uwezo wa kuunganishwa na internet. Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yanaweza kutokea pale unapo root simu yako.

Baada ya kuangalia mambo hayo muhimu twende sasa tukangalie programu ambazo zinaweza kuwa msaada kwako pale unapo amua kuchukua uamuzi wa ku-root simu yako.

1. Kingo ROOT

Kingo Root ni moja kati ya programu maarufu zaidi ambazo zinaweza kukusaidia kufanya root kwenye simu ya android. Programu hii inapatikana kwa njia ya kompyuta na kwa njia ya simu. Programu hii pia ni rahisi kutumia.

2. VRoot

Vroot ni programu nyingine kwa ajili ya kuroot simu ya Android, Programu hii inauwezo wa kuroot simu za aina mbalimbali, kwa mujibu wa kampuni iliyo tengeneza programu hii inadai kuwa programu hii inauwezo wa kuroot zaidi ya aina 8000 za simu za Android.

Hizi Hapa Apps Nzuri Kwaajili ya Watafutaji wa Ajira Rasmi

3. Root Genius

Root Genius ni programu nyingine ambayo inaweza kurahisha hatua nzima ya kuroot simu yako ya Android, Programu hii inaonekana kufanya kazi zaidi kwenye simu zinazotumia processor za Mediatek, simu hizo ni kama vile baadhi ya simu za TECNO, Huawei, iTel na Alcatel.

4. Unlock Root

Programu ya mwisho kwenye list hii ni programu ya Unlock Root, Programu hii ni sio rahisi sana kutumia na mbali ya kuroot simu yako pia programu hii inauwezo wa kusaidia zile simu ambazo zinatumia line ya mtandao mmoja. Programu hii ina maelekezo jinsi ya kutumia kwa kila simu hivyo ni muhimu kufuata hatua hizo kabla hujatumia programu hii.

Na hizo ndio programu nne ambazo zinaweza kukusaidia kuroot simu yako ya Android, Kumbuka unaweza kupakua programu hizi kupitia link ambazo zipo kwenye kila jina la programu husika. Kumbuka hatuta husika kama ukiharibu simu yako hivyo tumia programu hizi kwa uamuzi wako mwenye.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments