in

Instagram Sasa Kuruhusu Kuuza Bidhaa Kupita Stories

Sasa utaweza kuuza bidhaa zako kupitia sehemu ya Stories

Instagram Stories

Instagram imekuwa ikifanyiwa maboresho mapya kila mara, hivi karibuni instagram imetangazwa kuja na sehemu mpya ambayo itaruhusu watumiaji ku-post video za muda mrefu zaidi ya dakika moja na kitu kizuri zaidi ni kuwa inasemekana sehemu hiyo itaruhusu watumiaji kupata pesa kupitia matangazo ambayo yatakuwa yanapita kwenye video hizo.

Mbali na hilo, hivi leo instagram imetangaza kuwa sasa inakuja na aina mpya za stika ambazo zitaruhusu watumiaji wa mtandao wa instagram kupitia sehemu ya Stories kuuza bidhaa zao moja kwa moja kupitia sehemu hiyo. Stika hizo zitakuwa zinaonyesha bidhaa ambayo mteja anauza na pale mteja anapo gusa kwenye stika hiyo, atapelekwa moja kwa moja kwenye soko linalo uza bidhaa hizo.

Instagram imesema kwa sasa sehemu hiyo itakuwa inapatikana kwanza kwenye akaunti za kampuni kubwa za kuuza bidhaa mtandaoni na baadae sehemu hiyo itakuja kwa watumiaji wengine wa kawaida.

Tovuti za Kujifunza Kutengeneza Apps na Website Bure 100%

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.