Dawasco Kutumia Mfumo wa Malipo wa Kielektroniki wa (GePG)

Kwa kutumia mfumo huo Dawasco inatarajia kuokoa takriban Sh milioni 200
Dawasco GePG Dawasco GePG

Habari kutoka tovuti ya Lemtuz zinasema, Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), limesema linatarajia kuokoa takriban Sh.milioni 200 kila mwezi, kutokana na kuanza kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa malipo serikalini (GePG).

Mfumo huo umetajwa kulinufaisha shirika hilo kwa sababu utaondoa ulipaji wa tozo za kamisheni ya asilimia 4 kwa kila mihamala ya Shirika hilo, ambayo awali ilikuwa ikilipwa kwa wakala wakiwemo Maxcom na Selcom.

DAWASCO imesema mfumo huo unaanza kutumika kwenye malipo yote ya ankara za maji kuanzia leo, ambapo wateja watalipia kwa kutumia huduma za kifedha kwa simu za mkononi za M-PESA, tiGo PESA na Airtel Money.

Advertisement

Hayo yamesemwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja,wakati anazungumzia mfumo huo wa ulipaji kwa njia ya kieletroniki.  Luhemeja amesema GePG ni mfumo wa Serikali ambao unaunganisha taasisi zote za umma zinazotoa huduma na mteja wa huduma husika moja kwa moja bila kuwepo mtu wa kati.

“Katika mfumo huu mpya, malipo yatafanyika kwa kutumia kumbukumbu namba yaani Control Number ambayo ina tarakimu 12 na tutakuwa tunaitoa kwa mteja ili itumike kwenye malipo hayo kwa mihamala ya kifedha kwa njia ya simu.

”Shirika litapata fedha zake kwa wakati, kwa sababu zitakuwa zikiingia moja kwa moja kwenye akaunti yetu ya makusanyo na zitakazokuwa zimeokolewa kutokana na kupungua kwa gharama ya uendeshaji tutazirudisha kwenye utoaji huduma,” amesema.

Mhandisi Luhemeja ameongeza: “Kwa utaratibu huu DAWASCO haitohusika kwenye kulipia kamisheni ya mihamala itakayokuwa ikifanyika na badala yake, mteja atakuwa anakatwa kiasi kisichopungua asilimia moja ya kila mihamala ya malipo atakayofanya.”

Pamoja na ankara za maji, malipo mengine yatakayofanyika kwa mfumo wa GePG DAWASCO ni maunganisho mapya ya majisafi na majitaka, urejeshaji wa maji yaliyositishwa katika deni na manunuzi ya vitabu vya zabuni.

Imenakiliwa kutoka Tovuti ya Lemutuz

1 comments
  1. Hi kwa nn hamuelimish watu namna ya kulipa maji kwa kutumia no ya kumbukumbu, mtu unakuwa na pesa ila kulipa yaan haileeeki , au mnazan watu wote ni wafanyakaz wa dawasco? Badilikeni acheni kurahisisha mambo ,

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use