in

Hatimaye Chuo cha Tanzania cha DIT Kuanza Kuunda Roboti

Licha ya DIT, vyuo vingine ni pamoja na vyuo vya kenya, Ghana na Afrika Kusini

DIT kutengeneza Roboti
Picha na Parcrobotics.org

Hivi karibuni ripoti kutoka gazeti la mwananchi zinasema, Siemens ni miongoni mwa kampuni zin-azongoza kwenye uendelezaji wa taaluma ya artificial intelligence inayohamasisha ubunifu na uundaji wa roboti. Baada ya uzoefu wa miaka mingi, kam-puni hiyo imeamua kuongeza ushawishi wake Afrika kwa kuvijengea uwezo baadhi ya vyuo vikuu ili kuihamishia teknolojia hiyo barani humu.

Katika mpango huo, Chuo cha Teknolojia Dar es Salam (DIT) kinakuwa miongoni mwa vyuo 13 vya Afrika vilivyopewa mitambo ya kuunda roboti na kampuni ya Siemens. Mkuu wa kitengo cha uhusiano wa viwanda na taasisi wa DIT ambaye ni mratibu wa ushirikiano kati ya Siemens na chuo hicho, Dk John Msumba anasema uhusiano kati yao ulianza mwaka 2016.

Anasema mwaka huo, kampuni hiyo ilianzisha programu ya kutafuta mabalozi kwenye mataifa mbalimbali Afrika na taasisi hiyo ya elimu ya juu ikakidhi vigezo. Katika ushirikiano huo, Dk Msumba anasema: “Wanayo lab (maabara) itakayotumika kufundishia wanafunzi pamoja na wateja wa bidhaa zao. Ushirikiano huu unatoa fursa ya kuwa na wataalamu wa kusimamia viwanda vinavyohitaji teknolojia ya kisasa hata kuvifufua vilivyokufa.”

Hizi Hapa Tovuti Bora za Kupakua Movie Mpya (Bure)

Anasema kwenye hatua za awali msisitizo umeelekezwa kuandaa wataalamu wenye viwango vinavyokubalika kimataifa jambo litakalozishawishi kampuni za ndani au nje kuanzisha uzalishaji. “Wanafunzi wetu wameshatengeneza mitambo mingi lakini haijaendelezwa kwa kuwa DIT ni taasisi ya elimu si kampuni ya uzalishaji. Wakitokea wawekezaji, mambo mengi yatabadilika,” anasema.

Dk Msumba anasema Siemens wameshaleta Programmable Logic Controllers (PLC); mitambo inayotumika kuingiza maelekezo ya majukumu yatakayotekelezwa na roboti husika na kinachosubiriwa ni kompyuta maalumu zitakazofanikisha mawasiliano kati ya wataalamu na mashine husika. Mwezi uliopita, kampuni hiyo ilitangaza kutenga Dola 400,000 za Marekani (zaidi ya Sh896 milioni) kwa ajili ya kusambaza vifaa hivyo kwenye vyuo vikuu inavyoshirikiana navyo.

Ofisa mtendaji mkuu wa Siemens; kusini na mashariki mwa Afrika, Sabine Dall’Omo anasema tofauti ya maendeleo kati ya Afrika na mabara mengine inaweza kuondolewa kwa matumizi ya teknolojia hasa iliyotengenezwa sehemu husika kukabili changamoto zilizopo.

“Teknolojia ni muhimu Afrika lakini manufaa yake yataonekana endapo kutakuwa na mafunzo sahihi yanayotolewa kwa vijana na vifaa vya uhakika kufanikisha lengo lililokusudiwa,” anasema Dall’Omo.

Tovuti za Kujifunza Kutengeneza Apps na Website Bure 100%

Hata hivyo Vyuo vingine vitakavyo nufaika na mpango huo ni vya mataifa ya Tanzania, Ghana, Kenya na Afrika Kusini. Licha ya DIT, vingine vilivyo jumuishwa ni Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah (Ghana) na Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Dedan Kimathi (Kenya) pamoja na vyuo vikuu tisa vya Afrika Kusini.

Ripoti Kutoka Gazeti la Mwananchi

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.