in

Apple Kuzindua Leo Simu Mpya za iPhone 8 za Rangi Nyekundu

Simu hizi zitakuwa sehemu ya ushirikiano wa Apple na Shirika la RED

Apple Kuzindua Leo Simu Mpya za iPhone 8 za Rangi Nyekundu

Kampuni ya Apple hivi leo inatarajia kutangaza simu zake mpya za iPhone 8 pamoja na iPhone 8 Plus za rangi Nyekundu, Kwa mujibu wa tovuti ya Mac Rumors, kampuni ya Apple kila mwaka huzindua simu mpya za rangi nyekundu kutokana na ushirikiano wake na shirika lisilo la kiserikali la RED ambalo limejikita kusaidia kupambana na UKIMWI (HIV/AIDS) kwa nchi za Afrika.

Mwaka jana kampuni ya Apple ilizindua vifaa vyake vya iPad pamoja na simu za iPhone 7 na iPhone 7 Plus za rangi nyekundu, ikiwa kama alama ya ushirikiano huo wa kampuni ya Apple na shirika hilo la RED.

Hata hivyo, kwa sasa bado haijaulikana simu hizo zitauzwa kwa kiasi gani na bado zitakuwa na sifa na muonekano gani, lakini kwa mujibu wa mitandao mbalimbali inasemekana simu hizo zitakuja na sifa zile zile za kawaida za iPhone 8 na iPhone 8 Plus, lakini tofauti yake kubwa itakuwa ni muonekano wake wa rangi nyekundu pamoja na Bei zake. Kujua zaidi kuhusu simu hizo endelea kutembelea Tanzania Tech.

Mambo ya Kutegemea Kwenye Uzinduzi wa iPhone 14

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment