in

Hatimaye Mazungumzo Baina ya Serikali na Airtel Yaanza

Baada ya sakata la umiliki wa kampuni hiyo sasa mazungumzo yaanza

Hatimaye Mazungumzo Baina ya Serikali na Airtel Yaanza

Mazungumzo baina ya kampuni ya simu ya Airtel Tanzania pamoja na serikali Tanzania yameanza rasmi huku Mazungumzo hayo yakiwa yanalenga kufikia makubaliano yatakayokuwa na tija kwa pande zote mbili na kuimarisha sekta ya mawasiliano Tanzania.

Hata hivyo mazungumzo hayo yanakuja baada ya kuibuka utata hapo Desemba mwaka jana kuhusu mmiliki halali wa Airtel Tanzania, Serikali ikisema ndiyo mmiliki halali kwa sababu ubinafsishwaji wa kampuni hiyo haukufuata utaratibu madai ambayo yalikanushwa na kampuni ya Bharti Airtel.

Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi, Mazungumzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam, huku serikali ikiwakilishwa na mwenyekiti wa kamati maalumu iliyoundwa na Rais John Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, Upande wa Bharti Airtel unawakilishwa na mwanasheria mkuu wake anae julikana kwa jina la Mukesh Bhavnani.

Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 12, 2018 na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu, huku ikisisitiza kuwa mazungumzo hayo yana lengo la kufikia makubaliano yatakayokuwa na tija kwa pande zote mbili na kuimarisha sekta ya mawasiliano Tanzania.

Twitter Kufuta Alama ya Verified April 1 Mwaka Huu

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.