in

Video ya Uzinduzi wa Samsung Galaxy S9 Yavuja Angalia Hapa

Angalia video ya utangulizi wa uzinduzi wa Galaxy S9

Samsung Galaxy S9

Leo ni ile siku iliyokuwa inasubiriwa na watu wengi sana kwenye nchi mbalimbali, kwani leo ndio siku ambayo kampuni ya Samsung ina andika historia kwa mara nyingine kwa kutambulisha simu yake mpya ya Samsung Galaxy S9.

Lakini kabla ya kuzinduliwa kwa simu hii ni wazi kuwa, tayari tumesha jua karibia kila kitu kuhusu simu hii na kama haitoshi hivi leo ikiwa yamebakia masaa machache, kumevuja video ya utangulizi wa uzinduzi wa simu hiyo ambao unategemewa kuanza kufanyika saa 7:00 usiku siku ya leo kwa saa za Afrika Mashariki.

Video hii inaonyesha yale yote ambayo tulikuwa tumeyasema toka mwanzoni kama vile muonekano wa simu hiyo pamoja na yale yanayo tarajiwa kuja kwenye simu hiyo mpya. Mpaka sasa baadhi ya sifa ambazo tunazijua kuhusu simu hii ni kama vile –

Kioo cha Inch 5.8 chenye teknolojia ya QHD na Super AMOLED curved display (570ppi / 529ppi), Processor ya Qualcomm Snapdragon 845 (kwa simu za  marekani) na Samsung Exynos 9810 (kwa simu za UK). Pia Samsung Galaxy S9 Plus inategemewa kuja na ukubwa wa ndani wa GB 128 na RAM ya GB 6  na Galaxy S9 itakuwa na ukubwa wa GB 64 na RAM ya GB 4.

Tutakuwa tukionyesha uzinduzi huo mubashara kabisa kupitia Hapa hapa Tanzania Tech, hivyo kaa karibu na simu au kompyuta yako ili kuweza kujua yote yatakayo jiri kwenye mkutano huo wa Uzinduzi wa simu mpya ya Samsung Galaxy S9.

Simu za BlackBerry Kuacha Kufanya Kazi January 4 2022

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.