Samsung Yasitisha Toleo la Android 8.0 Oreo Kwenye Galaxy S8

Toleo hilo limesitishwa kwa muda ili kufanya marekebisho
Galaxy S8 Galaxy S8

Kampuni ya Samsung inaonekana kusitisha kwa muda kutoa toleo hilo jipya la Android Oreo 8.0 kwenye simu za Samsung Galaxy S8. Mapema wiki hii toleo hilo jipya lilianza kufikia baadhi ya simu kwenye nchi mbalimbali.

Baadhi ya nchi ambazo zilikuwa tayari zimesha anza kufikiwa na toleo hilo jipya ni pamoja na nchi za Turkey, Norway, UAE, India, Belgium, Germany, France, pamoja na Poland. Hata hivyo bado hakuna taarifa zozote kutoka kwa Samsung kuhusu sababu za kusimamisha kwa toleo hilo lakini ripoti kutoka tovuti ya SamMobile zinasema kuna uwezekano ni kuwa toleo hilo limepatikana kuwa na hitilafu na hivyo samsung imeanza kutengeneza toleo jipya kwaajili ya simu hizo.

Hivyo watumiaji wa Simu za Samsung Galaxy S8 itabidi kuendelea kusubiri mpaka hapo itakapo tangazwa tena kuhusu ujio wa toleo hilo jipya la Android Oreo 8.0 hopefully itakuwa ni siku za karibuni..

Advertisement

Update – 23/2/2018 Samsung imendelea kutoa Toleo Jipya la Android Oreo kwa simu za Samsung Galaxy S8 na S8 Plus.

Kwa habari zaidi hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na App Store vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use