in

Samsung Galaxy S8 Yaendelea Kupokea Toleo la Android Oreo 8.0

Watumiaji wa Galaxy S8 na S8 Plus kuendelea kupata toleo la Android Oreo

Samsung Galaxy S8 Yaendelea Kupokea Toleo la Android Oreo 8.0

Siku chache zilizo pita Samsung ilisimamisha kutoa toleo jipya la Android Oreo 8.0 kwenye simu za Samsung Galaxy S8 na Samsung Galaxy S8 Plus. Hii ilikuwa ni kutokana na sababu za toleo hilo jipya kuwa na matatizo mbalimbali.

Hivi leo Samsung imeanza tena kutoa toleo hilo jipya la Android Oreo 8.0 kwa simu hizo huku kwa sasa update hizo zikiwa zimekuja na build namba mpya. Kwa sasa toleo hilo jipya litawafikia hata wale ambao tayari walikuwa wamepata toleo jipya la awali kupitia awamu ya kwanza kabla ya Samsung kusimamisha utoaji wa update hizo.

Kwa wale ambao tayari walisha pata toleo la Android Oreo 8.0 kwenye simu zao za Galaxy S8 na S8 Plus, watapata toleo jingine ambalo litakuwa na maboresho ambalo toleo hilo litakuwa kwa makadirio ya ukubwa wa MB 500.

Kwa wale ambao hawakupata toleo hilo basi watapata toleo hilo jipya ambalo litakuwa na ukubwa wa kuanzia GB 1 na kuendelea. Kwa sasa update hizi zimeanza kupatikana nchini ujerumani na inategemewa siku za karibuni update hizi zitawafikia watumiaji wote ikiwa pamoja na watumiaji wa simu hizi hapa Tanzania.

Simu za BlackBerry Kuacha Kufanya Kazi January 4 2022

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.