in

Hizi Hapa Picha Nyingine za Simu Mpya ya Samsung Galaxy S9

Picha za simu mpya ya Samsung Galaxy S9 kabla ya kutoka

Samsung Galaxy S9

Ikiwa zimebaki siku sita tu hadi kuzinduliwa kwa simu mpya ya Samsung Galaxy S9, hivi leo kuvuja picha mpya za simu hiyo zikiwa zinaonyesha simu hiyo vizuri zaidi na kwa rangi tofauti.

Picha hizi zimevujishwa na mtandao wa winfuture, ambao unajulikana sana kwa kuvujisha picha mbalimbali za simu kabla ya kutoka kwake.

Simu hii inategemewa kuzinduliwa siku ya jumapili tarehe 25 mwezi huu wa pili na inategemewa kuja na sifa za kioo cha Inch 5.8 chenye teknolojia ya QHD na Super AMOLED curved display (570ppi / 529ppi), Processor ya Qualcomm Snapdragon 845 (kwa simu za  marekani) na Samsung Exynos 9810 (kwa simu za UK). Pia Samsung Galaxy S9 Plus inategemewa kuja na ukubwa wa ndani wa GB 128 na RAM ya GB 6  na Galaxy S9 itakuwa na ukubwa wa GB 64 na RAM ya GB 4.

Kujua zaidi yote yanayo tarajiwa kuja kwenye simu hii unaweza kusoma makala iliyopita inayo onyesha yote yanayo tarajiwa kuja kwenye Samsung Galaxy S9.

Fahamu Kuhusu RAM ya Ziada Kwenye Simu za Infinix NOTE 11

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.