YouTube Yaja na Vigezo na Masharti Mapya ya Matangazo

Sasa ni ngumu zaidi kuweza kutengeneza kipato kupitia Youtube
YouTube matangazo YouTube matangazo

Hivi karibuni mtandao wa Youtube kupitia tovuti yake, imetangaza kuongeza masharti kwenye mtandao wake juu ya Channel zinazo tegemea kuonyesha matangazo kwenye video zake, YouTube imefikia hatua hiyo baada ya baadhi ya watumiaji wa mtandao huo kuonekana kuvunja vigezo na masharti ya kuonyesha matangazo kwenye video ndani ya mtandao huo.

Hata hivyo sheria hiyo mpya sasa inawataka watu wote wanao miliki channel ya YouTube na wanataka kujipatia kipato kupitia matangazo yanayo onyeshwa na mtandao huo, kuhakikisha channel hiyo inayo Subscriber zaidi ya 1000 pamoja na video zilizo angaliwa kwa jumla ya masaa 4,000 kwa mwaka mzima.

Kwa kutimiza vigezo na masharti hayo ndipo channel hiyo itaweza kuanza kuonyesha matangazo na mmiliki wake kuanza kujipatia kipato. Hata hivyo sheria hiyo inatiliwa mkazo zaidi kwa watu ambao wanajiunga upya na mtandao huo, lakini pia YouTube imesema inatoa muda wa siku 30 kwa channel zilizopo ambazo hazija timiza vigezo hivyo kuhakikisha ina timiza vigezo hivyo kabla ya tarehe 20 mwezi wa pili mwaka huu 2018 bila hivyo matangazo hayo yataondolewa.

Advertisement

Mwaka jana YouTube ilileta sheria ya kuruhusu matangazo kwenye channel zenye jumla ya views 10,000, hii ikiendelea kuleta ugumu kwa channel zinazo anza kutengeneza kipato kutokana na matangazo yanayo onyeshwa na matandao huo.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

2 comments
  1. Hello,ningependa mtuwekee video nyengine ya kutengeza kipato kupitia Properleradds maana asa ivi ile smart link haipo na yataka uunge na website asa sifahamu nifanyeje

  2. naomba mnisaidie napataje kipato au nimekosea wapi mpaka sasa channel yangu haijaweza kuniingizia kipato.channel yangu ni Makambako TV.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use