in

Mambo Matano Uliyokuwa Hujui Kuhusu Mark Zuckerberg

Haya ndio mambo ambayo pengine ulikua hujui kuhusu Mark Zuckerberg

Mark Zuckerberg

Ni jumapili nyingine tena tunakutana kwenye makala za jewajuatech, hapa utapata kujua mambo mbalimbali yanayohusiana historia na teknolojia kwa ujumla.

Kwa jumapili ya leo hebu twende tukamuangalie kidogo Mark Zuckerberg, kwa wale ambao hawajui jina hilo basi Mark Zuckerberg ndio jina la kiongozi na muanzilishi wa mtandao wa Facebook. Kwa sasa Zuckerberg ni namba 5 kwenye list ya watu matajiri duniani akiwa na dhamani ya dollar za marekani $72.7 Bilion.

5. Hii ndio thamani ya T-shrit anazopenda kuvaa kila mara

Pengine ungedhani kwamba T-shirt anayopenda kuvaa Zuckerberg ni ya bei rahisi sana, lakini ni kinyume chake, T-shirt hiyo au niseme T-shirt hizo za rangi ya kijivu zinadhamni ya dollar za marekani $300 au $400 kwa T-shirt moja hii ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 700,00 au Tsh 900,000 hii sijasema mimi bali hii ni kwa mujibu wa tovuti ya businessinsider.com.

4. Bado kidogo angekuwa mfanyakazi wa kampuni ya Microsoft

Wakati Mark Zuckerberg yuko shule, alishawahi kutengeneza Application au programu ya muziki iliyokuwa inaitwa Synapse Media Player programu ambayo ilikua ina angalia nyimbo ambazo unapenda kuzisikiliza mara kwa mara kisha inatengeneza list ya nyimbo hizo. Kwa kipindi hicho hiyo ilikuwa ni teknolojia kubwa sana na Microsoft walikuwa wamesha tangaza nia ya dhati ya kununua programu hiyo pamoja na wanzilish wake yani Zuckerberg na Adam D’Angelo, lakini biashara hiyo haikufanikiwa sababu wote wagunduzi wa programu hiyo Zuckerberg na Adam D’Angelo waliamua kujiendeleza kieleimu kwa kujiunga na chuo.

3. Akiwa na miaka 12 Zuckerberg alishaanza kutengeneza programu

Pengine ungedhani kwamba juhudi za siku moja tu zinaweza kukufikisha mahali Zuckerberg alipo lakini ningependa kukwambia ni vyema ufunge mkanda kwani safari bado ni ndefu sana. Akiwa na miaka 12 tu Zuckerberg alitengeneza programu iliyoitwa ZuckNet ambayo ilikuwa maalumu kwaajili ya kumsaidia baba yake ambaye alikua ni daktari wa meno. Programu hiyo ilikuwa ikimsaidia baba yake kujua pindi wateja au wagonjwa watakapo kuja.

2. Alibuni rangi ya blue kwenye Facebook kutokana na ugonjwa wa macho

Kuna wakati unajiuliza mambo mengi sana kwa mfano hivi kwanini snapchat ni ya rangi ya njano au kwanini WhatsApp ni ya rangi ya kijani well… Kwa upande wa facebook sababu za Zuckerberg kutengeneza facebook ikiwa kwenye rangi ya blue ni kuwa, ana ugonjwa wa kuto ona baadhi ya rangi kuu kama nyekundu na kijani.

1. Zuckerberg anamiliki hisa asilimia 29 tu za mtandao wa Facebook

Pamoja na kuwa unaona asilimia 29 kama ni ndogo sana kwenye asilimia 100 lakini sasa yeye ndio tajiri namba 5 duniani. Najua ungependa kujua kampuni gani au watu gani wengine wanamiliki asilimia zilizobaki, baadhi ya watu na kampuni ni kama Microsoft inamiliki asilimia 1.6%, Accel Partners asilimia 10% na kampuni na watu wengine wengi unaweza kutazama list nzima HAPA.

Na hayo ndio mambo niliyo kuandalia leo kupitia kipengele hichi cha jewajuatech, Je ungependa kujua nini kuhusu teknolojia..? Tuandikie kwenye maoni hapo chini nasi tutafanya juhudi za kuhakikisha tunakufahamisha kupitia hapa hapa.

Kama unataka kujifunza zaidi na kupata habari za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload App yetu kupitia Play Store ambayo sasa imeboreshwa zaidi.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

7 Comments

  1. mimi niwashukuru sana kwa kunifungua akili na app hii ndio app ninayoipenda sana kwenye simu yangu. ila ninamaswali matatu. La kwanza nilitaka kujua kama ninaweza kusoma compyuta kwenye chuo chenu kwani mimi ni mwanafunzi wa saikolojia chuo cha mlimani (Udsm) ila sikusoma physics olevel. 02. nilitaka kujua ukiwa na blog unalipwa kiasi gani kulingana na watu wanaotembelea blog yako. yaani kiwango cha chini cha viewers na kiasi cha hela kwa siku. 03. nilitaka kujua jinsi ya kutengeneza video za katuni pamoja na program zake. (ningejisikia vyema kama ningepata majibu)

    • Wifredy Asante kwa kutembelea Tanzania Tech, Kujibu maswali yako sisi sio chuo wala taasisi ya kutoa elimu bali hapa ni sehemu ya kuhabarika na pengine kujifunza kuhusu Teknolojia. Kwa uoande wa jinsi ya kutengeneza katuni ni kuwa tunampango wa kuongeza vipengele kadhaa mwaka unaofuata na utaweza kujifunza mambo mengi yahusuyo teknolojia pamoja na maswala mazima ya Graphics. Hivyo endelea kutembele Tanzania Tech kila siku..