in

WhatsApp Kuja na Njia Mpya ya Kurekodi Meseji za Sauti

Sasa utaweza kuendelea kurekodi bila kushikilia kitufe cha kurekodi

WhatsApp Voice Message

Toka WhatsApp ilipo toa sehemu ya Voice messages hapo mwaka 2013, haijawahi kufanyiwa maboresho yoyote makubwa hadi kufikia sasa. Habari kutoka kwenye tovuti ya WABetaInfo zinasema kuwa WhatsApp inategemea kuboresha sehemu ya kurekodi sauti hasa kwenye mfumo mzima wa jinsi ya kurekodi sauti.

Maboresho hayo ni kuwa sasa utakuwa huna haja ya kushikilia kitufe cha kurekodi ili uweze kurekodi meseji za sauti, bali sasa baada ya kubofya kitufe cha kurekodi kwa sekude chake utaweza kuendelea kurekodi bila kushikilia kitufe cha kurekodi kwa kubofya huku unasogeza kitufe kipya ambacho kitaweza kufanya mtu aendelee kurekodi bila kushilia kwenye kitufe cha kurekodi.

Kizuri kuhusu ujio wa sehemu hiyo ni kuwa baada ya kuweza kubofya kitufe hicho ambacho kitakuwezesha kuendelea kurekodi, utaweza kuendelea kupitia baadhi ya meseji kwenye chat uliyopo angalia video hapo chini.

Sehemu hiyo inatarajiwa kuja hivi karibuni kupitia programu zote za WhatsApp za iOS na Android, Je nini maoni yako kuhusu sehemu hii unaona itakuwa msaada mkubwa kwako..? tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Pata Majibu ya Hesabu Yoyote kwa Kupiga Picha Maswali

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.