in

UC Browser Yaondolewa Kwenye Soko la Play Store Sababu Hii

Sababu za Google kuondoa App hiyo yenye download zaidi ya milioni 500

UC-Browser

UC Browser ni moja kati ya kisakuzi ambacho kimepata umaarufu mkubwa sana kwenye soko la Play Store, kisakuzi hicho kilikua na downloads zaidi ya milioni 500 kabla ya Google kuamua kuondoa App hiyo kwenye soko la Play Store  tena bila hata taarifa zozote.

Kwa wale ambao hawajui kuhusu UC Browser ni kuwa, kisakuzi hichi ni moja kati ya visakuzi vya mwanzo kabisa ambavyo vilikwepo enzi za simu za Nokia Symbian. Kisakuzi hichi kimetengenezwa na kampuni ya UC Union ya nchini China ambayo inamilikiwa na kampuni maarufu ya Alibaba Group.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Lakini zaidi ni kuwa kisakuzi hichi kimeweza kuwa maarufu sana kwa nchi kadhaa ikiwepo nchi ya India. Hata hivyo mapema mwezi wa nane mwaka huu, kisakuzi hicho kilituhumiwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo mashtaka ya programu hiyo kuchukua data za watumiaji wa programu hiyo kutoka india na kuzituma kwenye server za kampuni hiyo zilizopo nchini china.

Hata hivyo inasemekana kuwa hiyo sio sababu pekee ya kuondolewa kwa programu hiyo kwenye soko la Play Store, lakini inasemekana kuwa sababu ni kuwa programu hiyo imekua ikiweka matangazo mbalimbali ambayo yalikua na virusi na yalio kiuka utaratibu uliowekwa na Google kwenye soko lake la Play Store.

Lakini pia ripoti kutoka kwa mfanyakazi wa UC Browser Mike Ross, zinasema kuwa programu hiyo imetolewa kwa muda tu kutokana na utumiaji wa matangazo ambayo hayaruhusiwi ili kuweza kuongeza idadi ya watu ambao wana download programu hiyo kwenye soko la Play Store. Inasemekana kuwa programu hiyo ilikuwa na download nyingi nchini india kuliko hata kisakuzi cha Google Chrome.

Kwa sasa bado hakuna sababu kamili zilizotolewa na kampuni hiyo au wafanyakazi wa Google kuhusu kuondolewa kwa programu hiyo, lakini habari njema ni kuwa programu ya UC Browser Mini inapatikana Play Store na kama umekua ukitafuta kisakuzi hicho unaweza kutumia programu hiyo badala yake.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

UC Browser Yaondolewa Kwenye Soko la Play Store Sababu Hii
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps Muhimu kwaajili ya Mwezi wa Ramadhani (2024)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.