in

Instagram Sasa Kuruhusu Mtu Kuomba Kujiunga na Live Video

Sasa utaweza kumuomba rafiki yako kuwa nae live kwenye video moja

Instagram Live Mubashara

Hivi karibuni mtandao wa instagram ulileta mabadiliko ambayo yaliwezesha watumiaji wa mtandao huo kwenye sehemu ya Live Video kualikana na kuweza kuwa mubashara kupitia video moja.

Hivi karibuni mtandao huo umeboresha sehemu hiyo na kuleta uwezo wa mtu ambaye ni rafiki yako kuomba kujiunga na Live Video yako mara tu pale unapokuwa hewani. Mara tu unapokuwa una angalia video ya live ya mtu utaona kitufes kipya cha ‘Request‘ kilichoko chini kabisa karibia na sehemu ya Comment.


Bofya kitufe hicho kisha subiria ulio muomba aweze kukubali kisha moja kwa moja utaweza kuwa mubashara kabisa kwenye video moja na rafiki yako. Japo kuwa inawezekana watu wengi kuomba kuwa live na mtu fulani lakini maombi ya mtu mmoja tu kwa wakati ndio yanaweza kukubaliwa.

Sehemu hii inasemekan kuwa itakuwa maarufu sana sababu itasaidia watu maarufu kuweza kujiunganisha na wapenzi wao kwa njia ya video, kwa sasa tayari sehemu hii inaendelea kutoka kwenye Programu zote za Android na iOs na kama bado hujaiona ingia kwenye soko la Play Store au App store kisha angalia update za programu hiyo.

Je nini maoni yako kuhusu sehemu hii.. unahisi ni sehemu bora kuja kwenye app ya instagram au hii itaongeza usumbufu kwa watu maarufu..? tuambie kwenye maoni hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store pia usasahau kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kupata habari zote za teknolojia kwa njia ya Video.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.