in

Instagram Kuruhusu Watu Wawili Kuwa Live Kwenye Video Moja

Sasa Utaweza Kuunganisha Watu Wawili Kwenye Live Video Instagram

Live-with-a-Friend

Hivi leo mtandao wa instagram kupitia ukurasa wake wa habari imetangaza ujio wa sehemu mpya ya Go LIVE with a friend inayo tegemewa kuja kwenye programu za instagram za iOS na Android.

Sehemu hiyo itakuwezesha kumualika rafiki yako na wote mtaweza kuonekana kupitia simu mmoja kwa wakati huo huo. Kwa maana nyingine sehemu hiyo itawezesha marafiki wawili walioko mbalimbali na wanao tumia simu tofauti kuweza kuonyesha Live Video moja kupitia simu moja.

Pale rafiki anapo kuweka kwenye video hiyo basi moja kawa moja kioo cha simu yako kwenye programu ya Instagram kita gawanyika kwa juu na chini na kuonyesha video mbili ambazo zote zitakuwa Live kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa ukurasa huo wa Instagram Press, sehemu hiyo kwa sasa inajaribiwa na watu wachache na inategemewa kuja hivi karibuni kupitia programu za Instagram za Android na iOS. Kizuri zaidi kuhusu sehemu hii mpya ni kuwa utakuwa na uwezo wa kumtoa na kumunganisha rafiki yako yoyote kwa muda huo huo.

Apps za Kusaidia Kujibu Meseji WhatsApp (Bila Kushika Simu)

Sehemu hii inaweza kutumika zaidi kama unataka kunganisha watu wawili walioko mbali mbali na ni nzuri zaidi kwa watu wenye kurasa za kibiashara hasa zile ambazo huwa wanafanya mahojiano mbalimbali kwani sasa hii itawezesha wafuatiliaji kwenye mtandao wa instagram kuwa mubashara hata kama anae hojiwa yuko mbali.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : Instagram Press

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.