Sasa Utaweza Kutumia App ya Instagram ya Android Bila Internet

Sasa utaweza kutumia instagram kwenye simu yako ya android bila kuwa na internet
Instagram offline Instagram offline

Instagram kupitia mkutano wa F8 ulio anza rasmi hapo jana imetangazwa sehemu mpya kwenye programu hiyo maarufu yenye watumiaji zaidi ya milioni 600, sehemu hiyo ambayo itakuwezesha kutumia programu hiyo ya mfumo wa Android bila kuwa na Internet inategemewa kuja hivi karibuni.

Kuhusu jinsi sehemu hiyo itakavyofanya kazi, sasa mtumiaji ataweza kulike, kutoa maoni, kupitia post ambazo alisha pitia akiwa na internet pamoja na kupost kwenye programu hiyo bila kutumia internet post hizo zitawekwa draft na baadae unapo unganisha internet (data) kwenye simu yako ndipo vitu hivyo vinapo onekana live kwenye app hiyo ikiwa ni baada ya programu hiyo (ku-sync)  kuunganishwa na server za Instagram.

Sehemu hiyo inakuja hivi karibuni na inasemekana kuwa imetengenezwa maalum kwaajili ya nchi zenye uwezo mdogo wa internet. Hata hivyo Instagram imefanya maboresho kadhaa hivi karibuni ikiwa pamoja na kuweka sticker kwenye stories maarufu kama selfie stickers, pia uwezo wa kuweka picha zilizo hifadhiwa (saved picture) kwenye mtirirko maalum maarufu kama (collection).

Advertisement

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use