in

Jinsi ya Kutumia Kompyuta Yako Kupitia Simu Yako (Smartphone)

Jifunze njoa reahisi ya kutumia kompyuta yako kupitia simu yako ya mkononi

Kompyuta kwenye simu

Kuna wakati unatamani ungekuwa na uwezo wa kutumia smartphone yako kama kompyuta hivyo basi, kama wewe ni mmoja waliokua wanatamani hilo basi usijali kwani leo Tanzania Tech tunakuletea njia ya kutumia kompyuta yako kupitia simu yako ya mkononi au maarufu kama smartphone.

Kwa kuanza haijalishi unatumia simu yenye mfumo gani, iwe unatumia Android au iOS njia hii itaweza kufanya kazi vizuri kwenye simu na kompyuta yako kama utafuata hatua hizi kwa usahihi. Hakikisha tu unatumia browser ya Google Chrome, kama huna browser hiyo unaweza kudownload kupitia hapa kisha install kwenye kompyuta yako.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Baada ya kudownload na kuinstall browser ya Google Chrome kwenye kompyuta yako endelea kwa kudownload Extension ya Chrome Remote Desktop unaweza kudownload kwa kubofya hapo chini.

Unknown app
Price: Free

Install vizuri extension hiyo kwenye browser yako ya Google Chrome kisha baada ya instalation kukamilika utapelekwa kwenye Menu ya Google Chrome bofya kwenye Chrome Remote Desktop kisha utapelekwa kwenye ukurasa ambao sasa utatakiwa kuseti kompyuta yako. Nenda kwenye mahali palipo andikwa My Computer kisha bofya kwenye Enable Remote Connections baada ya hapo utatakiwa kuinstall programu ndogo ya MB 11 kwenye kompyuta yako na baada ya kumaliza utaona ukipelekwa ukurasa wa kuweka password hapa ni muhimu sana kumbuka kuweka password yako na usimuonyeshe mtu yoyote kisha baada ya hapo bofya OK kukamilisha, hatua inayofuata utaona jina la kompyuta yako likitokea kwenye programu hiyo.

Sasa ni wakati wa kuseti simu yako, moja kwa moja ingia  kwenye soko la Play Store kama unatumia Android au App Store kama unatumia iOS kisha download App ya Chrome Remote Desktop unaweza kudownload kwa kubofya hapo chini.

Chrome Remote Desktop – Android

Chrome Remote Desktop

Chrome Remote Desktop – iOS

Install programu hiyo kwenye simu yako kisha fungua na utaona jina la kompyuta yako baada ya hapo chagua jina ilo na moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wa kuweka password weka password yako kisha bofya Connect utaona kioo kisima cha kompyuta yako kikionekana kwenye simu yako, laza simu yako kwa upande kuweza kuona kioo kizima kisha unaweza kuendesha simu yako kwa kutumia touch screen ya kompyuta yako. Ukimaliza kutumia bofya Stop Sharing na utarudishwa kwenye kioo cha simu yako kama kawaida, vievile, unaweza kufanya chochote kwa kutumia njia hii.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

Jinsi ya Kutumia Kompyuta Yako Kupitia Simu Yako (Smartphone)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Simu Yako

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

5 Comments