in

Jinsi ya Kupata Laptop Yako Pale Inapo Potea au Kuibiwa

Fuata hatua hizi kama unataka kulinda laptop yako pale inapo ibiwa au kupotea

Laptop iliyopotea

Hivi sasa kuwa na laptop imekua ni kitu cha msingi sana hii inatokana na urahisi wa kubebeka kwa kompyuta hizo, lakini kutokana na urahisi huo kupotea au kuibiwa kwa kompyuta hizo kumekua ni rahisi sana ndio maana leo Tanzania Tech tunakuletea namna ya kulinda na kuitafuta laptop yako pale inapo potea au kuibiwa.

Moja kwa moja twende tukaangalie njia hizo za kulinda laptop yako, kumbuka ili kufanikisha hili hakikisha una internet kwenye kompyuta yako pamoja na uwezo wa ku-install programu kwenye kompyuta hiyo.

  • Jinsi ya Kuweka Programu ya Ulinzi kwenye Laptop Yako

Kwa kuanza tembelea tovuti ya Prey Project na tengeneza akaunti ya bure kupitia tovuti hiyo, kubali vigezo na masharti alafu kamilisha usajili wako kwa kutumia email na password yako kisha bofya sign up, baada ya hapo utaona umepelekwa kwenye ukurasa wenye ramani ya dunia ambayo haina kitu. Kwa upande wa kulia utona sehemu inayo kutaka kudownload programu ya prey kwenye kompyuta yako, hakikisha una download programu hiyo na install programu hiyo kwenye kompyuta yako.

  • Jinsi ya Kuset Programu ya Ulinzi Kwenye Laptop Yako
Jinsi ya Kuandika CV, Barua ya Kazi na Mifano ya CV (200+)

Baada ya kufanya hivyo bofya Finish ili kuwasha programu hiyo kisha chagua lugha alafu chagua ‘Existing user’ baada ya hapo tumia password pamoja na email (barua pepe) uliyotumia awali ili kuingia na kuunganisha laptop yako na ulinzi wa programu hiyo ya Prey baada ya kumaliza hatua zote utaona ujumbe ukikwambia laptop yako sasa ina ulinzi, Kumbuka kwa kutumia akaunti ya bure unaweza kulinda laptop tatu hivyo tumia programu hiyo kueka ulinzi kwenye laptop hizo.

  • Jinsi ya Kutafuta Laptop Iliyopotea

Baada ya kumaliza hatua zote hapo juu rudi kwenye tovuti ya preyproject.com alafu rudia kupakia ukurasa ule wenye ramani ya dunia na utaona laptop yako ilipo kwa muda huo. Sasa ili kupata laptop yako pale inapo potea ingia kwenye tovuti ya preyproject.com kisha ingia kwa kutumia email yako pamoja na password kisha chagua jina la laptop yako iliyopotea au kuibiwa kisha bofya kitufe kilicho andikwa ‘Set device to missing’ alafu bofya ‘Yes, my device is missing’.

Baada ya hapo utapata ujumbe ambao utaonyesha laptop yako ilipokuwa kwa mara ya mwisho na itaendelea kukuonyesha hata pale mtu anapotumia kompyuta yako, kumbuka programu hiyo inafanya kazi kwa nyuma hivyo sio rahisi mtu kujua kama programu hiyo ipo kwenye kompyuta yako.

  • Kufunga Laptop Yako Iliyo ibiwa au Kupotea
Jinsi ya Kupata Bidhaa za Amazon Bure Bila Kulipia

Hatua ya mwisho unaweza kufunga kabisa kompyuta yako ili mtumiaji asiweze kuangalia vitu vyako kwenye kompyuta hiyo iliyopotea au kuibiwa, ili kufanya hivyo bofya ‘Lock’ kisha chagua password unayo itaka kisha malizia kwa kubofya ‘Confirm’ baada ya hapo kompyuta yako itafungwa moja kwa moja mpaka password itakapo ingizwa kwenye laptop hiyo.

  • Ongeza Ulinzi kwa Programu za Android na iOS

Vievile programu hii inatumia App ya Android pamoja na iOS ambazo zinakusaidia kuona laptop yako popote pale ilipo kwa muda sahihi, unaweza kudownload programu hizo ili kuboresha ulinzi zaidi kwenye laptop yako. Bila shaka hatua hizi zitakuwa zimekusaidia endelea kutembelea Tanzania Tech ili kujifunza mengine mengi yahusuyo teknolojia.

Kwa Habari zaidi unaweza kudownload App ya Tanzania Tech kupitia Play Store ili kupata habari kwa haraka pale zinapotoka au unaweza kujiungana nasi kupitia channel yetu ya Youtube ili kupata habari za teknolojia na maujanja mbalimbali kwa njia ya Video.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Avatar

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment