Google Kuzindua Kifaa Kipya cha Google Wifi October 4

Kaa tayari kwa bidhaa mpya kutoka Google, kifaa kipya cha Google home Wi-Fi router kinakuja October 4
Google Wifi Google Wifi

Habari kutoka kwenye vyazo mbalimbali vya habari za teknolojia zina sema kuwa, huenda kampuni maarufu ya Google ikaleta bidhaa yake mpya itwayo Google Wifi. Google wifi ni kifaa ambacho kitatumiaka katika kusambaza internet ya kasi na yenye nguvu katika nyumba yako au hata kwenye ofisi yako. Hata hivyo kifaa hicho kinategemewa kuzinduliwa siku ya tarehe 4 mwezi october siku ambayo kampuni hiyo itakuwa ikifanya Tamasha la uzinduzi wa simu zake za Google Pixel pamoja na Google Pixel XL.

Mpaka sasa bado haijajulikana jinsi kifaa hicho kitakavyo fanya kazi au kitakua na kitu gani cha ziada ukilinganisha na Wi-Fi router zingine lakini habari hizo za tetesi ziliandikwa kuwa kifaa hicho kitauzwa kwa kati ya dollar za marekani $129 hadi dollar $150 ambayo ni sawa na shilingi za kitanzania Tsh 281,600.55 na Tsh 327,442.50 bei hizo ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya tarehe 24-09-2016. Kingine kilichosemwa kuhusu kifaa hicho kipya nia rangi kwani kifaa hicho kinategemewa kuja na rangi nyeupe na kitakuwa na mfanano kidogo na kile cha Amazon Echo Dot. Vilevile Google Wifi integemewa kuzinduliwa sambamba na Google Home pamoja na Google 4K ‘Chromecast Ultra’ kifaa kingine kutoka kampuni hiyo maarufu ya Google.

Ili kufuatilia habari za kifaa hicho cha Google Wifi pamoja na Kuangalia Tamasha zima la Uzinduzi wa Vifaa hivyo vyote endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use