in

Jinsi ya Kuweka Subtitle Kwenye Filamu Yoyote

Jinsi ya Kuweka Subtitle Kwenye Filamu Yoyote

Siku hizi watu wengi wamezoea kuangalia filamu uku wakisoma tafsiri ya maneno yake kwa chini ya filamu, hata filamu za tanzania siku hizi zinakua na subtitle. Lakini filamu nyingi tunazo pakua mitandaoni nyingi huwa hazina subtitle je unafanyaje na unatamani kuangalia na kuielewa filamu flani uliyo pakua mtandaoni.?

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Ifuatayo ni njia rahisi sana ya kupakua subtitle bila hata kutumia nguvu wala muda wa kutafuta subtitle hiyo kwenye google, kumbuka ili uweze kufanya hivi unatakiwa kuwa na internet na bando ambayo kiwango cha chini kiwe kama MB50 hivi ili uweze kupakua progamu maalumu kwa kupakua subtitle.

Hatua ya kwanza bofya link hii hapa [button type=”primary” text=”BS Player” url=”http://www.bsplayer.com/bsplayer-english/download-free.html” open_new_tab=”true”] kisha utapelekwa moja kwa moja kwenye blog ya programu hiyo ambapo shusha chini kidogo kisha bofya sehemu iliyo andikwa “Download Free” baada ya hapo utaanza kupakua programu hiyo moja kwa moja kwenye kompyuta.

Ukisha maliza kupakua progamu hiyo hakikisha kompyuta yako inaendela kunganishwa na internet kisha anza kuhifadhi (install) programu hiyo kwenye kompyuta yako hakikisha unapakua kila kitu ambacho programu hiyo inahitaji, kisha kamilisha kuhifadhi programu hiyo kwenye kompyuta yako kwa kubofya kitufe kilicho andikwa “Finish”.

Ukiwa umemaliza hatua hizo utakuwa uko tayari kuanza kupakua subtitle kirahisi kabisa bila kupoteza muda, ili kukufanya uelewe zaidi programu hii ni “video player” ambayo inauwezo wa kutafuta subtitle yenyewe kwenye mtandao bila wewe kuangaika hata kidogo hivyo basi unachotakiwa kufanya ni kucheza filamu zako kwa kutumia programu hiyo ya BS Player na yenyewe itafanya kazi ya kutafuta na itakuruhusu wewe kudownload subtitle moja kwa moja kwenye filamu yako. Pia kumbuka kuna wakati kama zilivyo programu zingine inaweza isipate subtitle au wewe ukapakua subtitle ambayo haiendani na maneno ya filamu yako, ukiona hivyo usijali unaweza ukapakua au ukatafuta subtitle yako kwa mara ya pili kwa kubofya Subtitle > Check subtitle online > All hapo utaweza kupakua tena subtile ya filamu yako.

Kama ilivyo kawaida unaweza ukaangalia video hiyo hapo juu ili kujifunza zaidi, pia usisite kutuandikia comment kama kuna mahali umekwama na tutakusaidi bure kabisa na kwa haraka.

Jinsi ya Kuweka Subtitle Kwenye Filamu Yoyote
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kupata File Lolote kwa Haraka (MP3,MP4,ZIP,PDF,ISO)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments