Bei za iPhone 16, iPhone 16 Pro, na iPhone 16 Pro Max nchini Tanzania ni zipi?
Bei ya iPhone 16 Tanzania
- Best Answerset by AmaniJoseph
Bei za iPhone 16, iPhone 16 Pro, na iPhone 16 Pro Max nchini Tanzania zinategemea uwezo wa kuhifadhi data (storage) wa kila toleo. Hapa chini ni jedwali linaloonyesha bei kwa kila toleo na uwezo wake:
Toleo | Uwezo wa Uhifadhi | Bei (TZS) |
---|---|---|
iPhone 16 | 128 GB | 2,500,000 - 2,600,000 |
256 GB | 2,800,000 - 3,000,000 | |
512 GB | 3,200,000 - 3,400,000 | |
iPhone 16 Pro | 256 GB | 3,500,000 - 3,800,000 |
512 GB | 4,000,000 - 4,200,000 | |
1 TB | 4,500,000 - 4,700,000 | |
iPhone 16 Pro Max | 256 GB | 3,800,000 - 4,000,000 |
512 GB | 4,200,000 - 4,500,000 | |
1 TB | 4,700,000 - 5,000,000 |
Kumbuka: Bei hizi zinaweza kutofautiana kulingana na duka na eneo ulipo.
Wauzaji wazuri wa iPhone 16 wanao aminika kwa Dar es salaam ni wapi unaweza kuweka list hapa..?
Kwa kuzingatia uzoefu wangu binafsi naona Phonepoint Dar, wana huduma bora. Pia, iphone_ogtz, Elite Computers, na TheTech360 wanaonekana kuwa na sifa nzuri kulingana na maelezo yao. Kabla ya kufanya manunuzi, ni vyema kupitia maoni ya wateja wengine na kuhakikisha uhalali wa duka husika ili kupata bidhaa halisi na huduma bora. Binafsi nimefanya manunuzi kupitia Phonepointdar hivyo naweza kuwaamini. Angalia akaunti zao za Instagram na angalia na maoni mengine ya watu.
Jina la Muuzaji | Akaunti ya Instagram |
---|---|
Phonepoint Dar | @phonepointdar |
iphone_ogtz | @iphone_ogtz |
Elite Computers | @elitetanzania |
TheTech360 | @thetech360 |
Kumbuka kufanya utafiti wa kina na kusoma maoni ya wateja wengine kabla ya kufanya manunuzi ili kuhakikisha unapata bidhaa halisi na huduma bora.
Hii iko poa ila kuna wa mikoani pia tunapata wapi hizi simu sehemu ya kuaminika, maana kuna sehemu nyingine pia nasi hatuna watu wengi wa kuaminika..?
- Edited
DalaliMkononi sijui kama kuna wauzaji wengi wa simu mikoani kama ilivyo dar es salaam hasa iphone, unaweza kuagiza hapa dar es salaam then ukaletewa mkoani.