TCRA Yafafanua Usajili wa Laini kwa Kutumia Alama za Vidole

Airtel imekuwa ya kwanza kutoa ufafanuzi juu ya usajili huo utakavyokuwa
Usajili wa Laini Usajili wa Laini

Hivi karibuni taarifa kutoka kwenye mitandao ya simu zilibainisha kuwa, sasa kutakuwepo na aina mpya ya usajili wa laini za simu za mkononi ambao utahusisha alama za vidole.

Aidha katika taarifa hiyo ambayo ilikuwa ikitolewa na mitandao mbambali ya simu kupitia meseji za ujumbe mfupi, kumekuwa na maswali mengi sana na wengi wakiwa wanataka kujua juu ya utaratibu mzima wa usajili huo utakavyokuwa.

Sasa hivi leo taarifa kupitia tovuti ya mwananchi zinasema kuwa Kaimu meneja mawasiliano kwa umma wa mamlaka ya mawasiliano ya Tanzania TCRA, Semu Mwakyanjala alisema walishafanya majaribio kuhusu mfumo huo na kuona unafaa hivyo watoa huduma za simu za mkononi wame ruhisiwa kuanza kutumia.

Advertisement

Hata hivyo meneja huyo alisema kuwa mfumo huo unaotumia alama za vidole na picha ni wenye uhakika na ambao ni vigumu mtu kughushi. “Huu ni usajili wa kielektroniki ambao unaiwezesha kampuni na mamlaka kupata taarifa mbalimbali za mteja kwa muda mfupi,” alisema kaimu meneja huyo wa TCRA.

Katika kupata ufafanuzi wa jinsi usajili huo utakavyo kuwa, mwandishi wa tovuti ya mwananchi ali-wasiliana na meneja uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando ambaye alimwambia mwandishi huyo kuwa, Airtel itanza kufanya usajili huo mpya kwa hatua ya majaribio hivi karibuni.

Meneja huyo wa Airtel Tanzania aliendelea kusema, kupitia mpango huo wa majaribio wataanza kusajili katika mikoa minne ya Dar es Salaam, Pwani, Iringa na Singida. Pia, uta fanyika Zanzibar na kote huko usajili huo utafanyika kwa awamu hiyo kwa wateja wapya.

Meneja huyo aliendelea kuongeza kuwa, baada ya hatua hiyo kukamilika kampuni hiyo itaendelea na kuwasajili watu wengine hata ambao walisha sajiliwa awali kwa nia ya kuboresha zaidi mfumo huo.

Mpaka sasa bado hakuna taarifa zaidi kutoka kwa mitandao mingine ya simu kuhusu jinsi itakavyo fanya usajili huo mpya, lakini endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuletea taarifa zaidi pindi tutakapo pata utaratibu huo kutoka kwa makampuni mengine ya simu.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

4 comments
  1. Maoni*Je ambao hawana vitambulisho na wanahtaji mawasiliano itabidi wakae kimya bila kuwasiliana au mtatusaidiaje

  2. Maoni*jamen Sasa Mufumo Wa Kusajili Rain Ukibadilishwa Tutatumia Sumartphone Kama Kawaida Au Itakueje

  3. Maoni*line yangu nimesajii Vida shop nashangaa naambuwa haijasajiliwa namba yangu ni 0759439946 Vida na airtel ni 0784961166 namba yangu ya nida ni

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use