Hizi Hapa Settings za Samsung Ambazo Ulikuwa Huzijui

Fanya mambo mengi kwa kupitia Settings hizi za Samsung
Hizi Hapa Settings za Samsung Ambazo Ulikuwa Huzijui Hizi Hapa Settings za Samsung Ambazo Ulikuwa Huzijui

Ni wazi kuwa simu nyingi za Android zinakuja na settings nyingi mbalimbali ambazo sio zote ambazo unaweza ukawa unazijua. Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha settings ambazo huwenda ulikuwa huzijui ambazo zinapatikana kwenye simu yako ya Samsung.

Kumbuka ni muhimu kuwa na mfumo mpya wa Android, au kuwa na angalau simu ya Samsung yenye mfumo wa Android kuanzia Android 10 na kuendelea. Pia baadhi ya Settings hizi zinaweza kuwa zinapatikana kwenye simu nyingine hivyo unakaribishwa kutafuta sehemu hii kwenye simu yako yoyote ambayo sio Samsung.

Basi baada ya kusema hayo moja kwa moja twende kwenye makala hii ili ufahamu settings mpya ambazo ulikuwa huzijui zinazo patikana kwenye simu yako ya Android ya Samsung.

Advertisement

Washa Subtitle Kwenye Video Yoyote

Samsung inakuja na sehemu mpya ambayo inakuruhusu kuwasha subtitle kwenye video yoyote pale unapocheza video hiyo kwenye simu yako. Sehemu hii hufanya kazi kwenye video yoyote ikiwa pamoja na video za YouTube. Washa sehemu hii kupitia sehemu ya Settings > Accessibility > Hearing enhancements > Live Caption.

Hizi Hapa Settings za Samsung Ambazo Ulikuwa Huzijui

Kama utakuta sehemu hii imezimwa unatakiwa kudownload update kwenye simu yako ambayo itaonekana kwenye ukurasa huu, bofya download kupakua update hiyo ambayo huwa na MB 40 tu.

Ongeza au Punguza Size ya Keyboard

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hupata shida ya kutumia simu kwa mikono miwili hasa unapokuwa una andika meseji basi kupitia simu yako ya Samsung unaweza kupunguza au kuongeza ukubwa wa keyboard yako. Ili kupata sehemu hii ingie kwenye Settings > General Management > Samsung Keyboard settings > Size and transparency.

Hizi Hapa Settings za Samsung Ambazo Ulikuwa Huzijui

Pandisha juu, au vuta kushoto au kulia kuweza kupunguza au kuongeza Size ya keyboard ya simu yako. Pia unaweza kuvuta katikati kuweza kuchagua mahali ambapo keyboard itakuwa inatokea.

Tumia Sehemu ya Fingerprint Kufungua Notification

Kama simu yako inayo sehemu ya fingerprint kwenye nyuma pengine sehemu hii inaweza kukusaidia sana, kupitia sehemu ya fingerprint kwa kuslide sehemu hiyo kwenye chini utaweza kufungua sehemu ya Notification na hii itakusaidia sana kama unatumia simu yako kwa mkono mmoja.

Unaweza kupata na kuwasha sehemu hii kupitia sehemu ya Settings > Advanced features > Motions and gestures > Finger sensor gestures. Kisha washa sehemu hiyo.

Hizi Hapa Settings za Samsung Ambazo Ulikuwa Huzijui

Baada ya kuwasha sasa kwenye sehemu ya fingerprint ya simu yako papasa sehemu hiyo kwa kwenda chini utaona Notification imefunguka, na pia ukipapasa kwa kwenda juu utaona sehemu hiyo imefunga moja kwa moja.

Zuia Ukurasa Mtu Asifungue Kitu Kingine

Kama wewe ni mmoja wa watu wenye watoto najua hii itakusaidia sana. Kama watoto wako au mtu mwingine yoyote amekuwa akiomba simu yako kufanya jambo fulani, kwa mfano kwa watoto wanapenda kuomba simu kuangalia katuni au kucheza game.

Mara nyingi watoto hupenda kugusa gusa simu na usipokuwa muangalifu utakuta yupo kwenye meseji za WhatsApp au kwenye Gallery. Sasa kuzuia hii unaweza kufanya screen ya simu yako ibaki sehemu moja na mtu asiweze kutoa mpaka utakapofanya hatua fulani.

Unaweza kuwasha sehemu hii kupitia Settings > Biometrics and security > Other security settings > Pin windows. Kiswa washa sehemu hiyo na weka On.

Hizi Hapa Settings za Samsung Ambazo Ulikuwa Huzijui

Baada ya kuwasha sehemu hii ya Pin Windows sasa kila mara mtu au mtoto atakapo taka kucheza game kwenye simu yako moja kwa moja fungua Game hiyo kisha bofya kitufe cha Recently, ambacho huwa karibu na kitufe cha back. Kisha bofya kitufe cha pin kinacho onekana kwa pembeni, au kama unatumia gesture unaweza kubofya Icon ya app kicha chagua pin this app.

Hizi Hapa Settings za Samsung Ambazo Ulikuwa Huzijui

Washa Menu ya Ziada Kutumia Simu kwa Haraka

Kama unataka kutumia simu yako kwa haraka na kwa mkono mmoja, kupitia settings unaweza kuwasha menu ya haraka ambayo itakusaidia kuendesha simu yako kwa mkono mmoja na kwa haraka. Unaweza kuwasha sehemu hiyo kupitia sehemu ya Settings > Accessibility > Interaction and dexterity > Assistant menu.

Hizi Hapa Settings za Samsung Ambazo Ulikuwa Huzijui

Baada ya kuwasha sehemu hiyo moja kwa moja utaweza kuona kibonyezo chenye vitu kama hivyo vilivyofunguka hapo juu ya ukurasa huo, vibonyezo hivyo ni pamoja na sehemu ya kuchukua screenshot, kitufe cha back, Home na Recently na vibonyezo vingine vingi.

Na hizo ndio sehemu chache tu ambazo inawezekana ulikuwa uzijui kwenye simu yako ya Samsung. Kama unataka kujua sehemu nyingine zaidi hakikisha unatembelea channel yetu ya Tanzania tech ili kujifunza zaidi kwa vitendo.

Kwa maujanja zaidi unaweza kusoma hapa kujua Menu za siri ambazo ulikuwa uzijui kwenye simu yako ya Android. Kwa habari zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use