in

Gazeti Tanzania : Soma Habari Mpya Bila Internet (Android)

Soma habari zote kutoka Tanzania bila kutumia Internet kila mara

Gazeti Tanzania : Soma Habari Mpya Bila Internet (Android)

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao unataka kupata habari kwa wakati na kwa haraka basi app ya Gazeti inakupa uwezo wa kusoma habari mbalimbali za hapa Tanzania kutoka kwenye vyanzo bora hapa Tanzania.

Pamoja na kuwa unawaza kuwa hitaji app nyingine ya habari kwenye simu yako lakini hebu nipe dakika moja nikueleze vizuri kuhusu gazeti app

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot

Najua wewe kama watu wengine hutumia Opera News kupata habari lakini wote tunakubaliana kuwa app ya Opera News imekuwa ikileta habari ambazo kuna wakati unakuta ni habari za miaka hata miwili iliyopita.

Mbali na hayo Pia wakati mwingine app ya Opera News huleta makala nyingi zilizo tafsiriwa ambazo ukweli kuna wakati mwingine hazina maadili, japo kuwa makala hizo zinapendwa na watu wengi sana hapa Tanzania hasa vijana.

App ya Gazeti inakupa uwezo wa kusoma habari bila Internet na pia utaweza kupata habari mpya kila siku ikiwa pamoja na kusoma magazeti, kusikiliza Radio na vipindi mbalimbali bila kusahau uwezo wa kuanzisha na kusoma mijadala kupitia Jamii Forums. Bila shaka mambo kama hayo huwezi kuyapata kupitia app ya Opera News

Hayo ni baadhi ya mambo tu yafuatayo ni mambo mengine zaidi unayoweza kupata kupitia app ya Gazeti..

 • Utaweza kusoma habari kutoka kwa vyanzo zaidi ya 20 vinavyo aminika
 • Utaweza kisikilza radio kama Clouds FM, Global Radio, Radio One, E.Fm na vipindi mbalimbali, pia utaweza kudownload vipindi hivyo kwaajili ya kusikiliza baadae.
 • Utaweza kusoma mijadala kupitia tovuti ya jamii forums, pia utaweza kuanzisha na kujibu mijadala hiyo kwa urahisi kupitia app ya Gazeti App.
 • Utaweza kusoma habari bila Internet, yani baada ya kufungua app hii subiri iweze kusave habari mpya kisha unaweza kuzima Internet na kuendelea kusoma habari zote zilizopo.
 • Pia utaweza kupata muonekano wa Giza ambao utasaidia kulinda macho yako hasa wakati wa usiku.
 • Utaweza kusoma habari kutoka mtandao wa Instagram, Twitter Telegram na hivi karibu utaweza kuangalia video za TikTok.
 • Pamoja na mambo mengine mengi.

Kwa kifupi app ya Gazeti ni app ya tofauti sana ya habari kwa hapa Tanzania, na kama huniamini unaweza kujaribu app hii kupitia link hapo chini.

Kama unaona huitaji kuwepo na app hii basi unaweza kujaribu tovuti ya Gazeti kupitia link hapa, kumbuka kupitia tovuti hutoweza kusoma habari kutoka mitandao ya kijamii ikiwemo na jamii forums.

Kama umependa ulichosoma na unataka kujaribu app ya Gazeti basi unaweza kudownload app hii kupitia Link hapo chini.

Gazeti - Tanzania
Gazeti - Tanzania
Developer: Tanzania Tech
Price: Free

Download App ya Gazeti Hapa

Kama una maon, maswali au ushauri unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Apps Nzuri Kwa Simu za Android Zilizopo Rooted

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.