in

Sifa za Muhimu za Simu Mpya ya Infinix Hot 10 Play

Infinix Hot 10 Play inakuja na battery kubwa yenye uwezo wa kudumu zaidi ya siku moja

Sifa za Muhimu za Simu Mpya ya Infinix Hot 10 Play

Infinix HOT 10 Play ni simu mpya katika toleo la HOT iliyobeba sifa kubwa katika upande wa battery ikiwa na mAh 6000 na processor Helio G35 kwajili ya uchezaji games kwa muda mrefu pasipo kuzima chaji. HOT 10 Play ina kioo kipana cha nchi 6.89 na kamera yenye selfie 8MP kwajili ya kufurahia picha mahali popote na wakati wowote.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Battery:

Infinix ina mAh 6000 za battery lakini je ni vipi battery hii inaweza kukufaidisha, battery ya HOT 10 Play inakupa nafasi yakufanya vitu vingi kama vile kucheza games, kuangalia movie, kusikiliza music nakadhalika pasipo kukata chaji.

Memory:

HOT 10 play inapatika ikiwa na memory ya GB2/32 na GB4/64 ni wakati gani utatambua hii ni simu muhimu kwako nipale unapokuwa na vitu vingi kama vile picha, video, vitabu vya kujisomea au hata application mpya na ungependa kuhifadhi pasipo shida ya kuletewa ujumbe wa Memory imejaa.

Sifa za Muhimu za Simu Mpya ya Infinix Hot 10 Play

Wigo wa kioo:

Hot 10 Play eneo lake la mbele limetawaliwa na wigo mpana wa kioo cha nchi 6.89 kwajili ya kuendelea kukuweka karibu na matukio mbalimbali kama vile mpira, tamthlia ukiwa katika pirika pirika za kila siku na wakati wa uchukuaji picha pia inachukua picha kwa ukubwa zaidi.

Kamera:

Hot 10 Play imekuja ikiwa na MP8 mbele pamoja na flash nyuma ikiwa na MP13 na flash. Kamera za Infinix Hot 10 Play zinakupa picha zinazoendana na uhalisia wa mazingira kwa wakati wowote haijalishi ni kwenye jua kali au kwenye kiza kinene.

Processor:

Hiki ni kifaa muhimu sana katika simu yoyote endapo processor itakuwa haina uwezo basi hautaweza ifurahia simu yako. Hot 10 Play ina processor ya Helio G35 yenye kuifanya simu iwe nyepesi wakati wa utumiaji kama vile uchezaji games nakadhalika.

Infinix HOT 10 Play inapatikana katika maduka ya Tigo na Infinix nchini kote.

Amani Joseph

Sifa za Muhimu za Simu Mpya ya Infinix Hot 10 Play

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Ifahamu Simu Sahihi Kwa Content Creators

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.