in

Infinix Yazindua Simu Mpya za Infinix Note 8 na Note 8i

Zifahamu hizi hapa sifa na bei ya simu mpya za Infinix Note 8 na Infinix Note 8i

Infinix Yazindua Simu Mpya za Infinix Note 8 na Note 8i

Kampuni ya Infinix hapo jana ilifanikiwa kuzindua simu zake mbili ambazo ni matoleo mpya ya simu zake za Note, yaani Infinix Note 8 na Infinix Note 8i. Simu zote mbili zinakuja na sifa zinazo karibia kufanana isipokuwa vitu vichache kama kamera za mbele na nyuma pamoja ukubwa.

Infinix Yazindua Simu Mpya za Infinix Note 8 na Note 8i

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kioo

Tukiongelea ukubwa, Infinix Note 8 inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.95, wakati Note 8i inakuja na kioo cha inch 6.78. Simu zote zimetumia teknolojia ya IPS LCD kutengeneza vioo hivyo na pia simu zote zinakuja na resolution inayo fanana ya pixel 720 kwa 1640.

Kamera ya Mbele na Nyuma

Kwa upande wa kamera ya mbele, Infinix Note 8 inakuja na kamera mbili za selfie, kamera moja ina uwezo wa Megapixel 16 huku kamera nyingine ikiwa na uwezo wa Megapixel 2. Note 8i inakuja na kamera moja kwa mbele yenye uwezo wa Megapixel 8. Simu zote zinakuja na Flash ya mbele ya Dual-LED.

Kwa nyuma simu hizi zinakuja na kamera nne kila moja, lakini kwa upande wa Note 8 yenyewe inakuja na kamera kuu ya Megapixel 64 na nyingine tatu zikiwa ni Megapixel 2 kila moja. Infinix Note 8i yenyewe inakuja na kamera kuu ya Megapixel 48 huku kamera nyingine zikiwa Megapixel 2 kila moja.

Sifa za Ndani

Kwa upande wa sifa za ndani Infinix Note 8 na Note 8i hazina tofauti, Simu hizi zinatumia processor ya Mediatek Helio G80 (12 nm) yenye uwezo wa CPU ya hadi Octa-core (2×2.0 GHz Cortex-A75 & 6×1.8 GHz Cortex-A55). CPU hiyo inapewa nguvu na RAM ya GB 6 pamoja na ROM ya GB 128. Unaweza kuongeza uhifadhi wa simu hii kwa kutumia memory card ya hadi GB 128.

Viunganishi

Kwa upande wa viunganishi, Simu zote pia zinalingana kwani zote zinakuja na sehemu ya ulinzi ya fingerprint ambayo ipo kwa pembeni, na pia simu zote zinakuja na Radio FM pamoja na sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack.

Battery

Tukiangalia kwenye upande wa battery Infinix Note 8 na Note 8i zote zinakuja na battery ya 5200mAh, battery ambayo inasaidiwa na teknolojia ya fast charging (18W) ilikufanya iweze kujaa kwa haraka. Mbali na hayo simu hii inakuja kwa rangi tatu tofauti yaani rangi ya Gray, Blue, na Green.

Upatikanaji na Bei

Kwa upande wa bei, Infinix Note 8 na Note 8i zinategemewa kupatikana hivi karibuni na bei ya simu hizi inakadiriwa kuwa bei nafuu. Unaweza kusoma hapo chini kujua bei ya simu hizo kwa hapa Tanzania.

Infinix Yazindua Simu Mpya za Infinix Note 8 na Note 8i
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Infinix na JBL Waungana Tena Na Sasa Ni Infinix Note 40

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.