in

Hizi Hapa Picha Halisi za Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Simu hii inaonekana kufanana muonekano na simu mpya ya Tecno camon 15 Pro

Hizi Hapa Picha Halisi za Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Wakati tukiwa bado tunasubiri simu mpya za Tecno Camon 15 na Camon 15 Pro zifike hapa Tanzania, hivi leo picha zimevunja mtandaoni zikionyesha muonekano halisi wa simu mpya ya Infinix S5 Pro.

Kwa mujibu wa tovuti ya GSMArena, picha hizo ambazo zinasemekana kuwa ni za Infinix S5 Pro, zinaonyesha simu hiyo ikiwa inafanana kabisa na simu mpya ya Camon 15 Pro ambayo imezinduliwa siku za karibuni huko nchini India.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Hizi Hapa Picha Halisi za Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Mbali na muonekano, pia kwa mujibu wa GSMArena, kamera kuu ya simu hii inatarajiwa kuwa na uwezo wa Megapixel 48 huku kamera nyingine mbili zikiwa bado hazijajulikana. Kwa ujumla simu hii inasemekana kuja na kamera tatu kwa nyuma huku kamera ya selfie ikiwa kwenye mota maalum inayo ficha kamera hiyo ndani ya simu hiyo pale inapo kuwa haitumiki.

Hizi Hapa Picha Halisi za Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Kwa upande wa kioo Infinix S5 Pro pia inaonekana kuja na kioo cha Full View ambacho kinakuja na ukingo mdogo hasa kwa juu kutokana na kuhamishwa kwa kamera ya mbele au Selfie kamera. Kwa sasa bado haijajulikana ukubwa wa kioo hicho, ila pengeine tegemea kuwa simu hii inaweza ikiwa inafanana kila kitu na Tecno Camon 15 Pro.

Hizi Hapa Picha Halisi za Simu Mpya ya Infinix S5 Pro

Awali ilikuwa ikisemekana kuwa, simu hii inaweza kuzinduliwa mwezi huu wa pili lakini kutokana na kuwa simu mpya za Tecno Camon 15 ndio zimetoka mwezi huu, hivyo kwa sasa inawezekana simu hii mpya kutoka infinix ikatoka mwezi wa tatu au mwezi wa nne mwanzoni. Kuhakikisha hupitwi sifa kamili pamoja na bei ya simu hii, endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Angalia Uzinduzi wa iPhone 15 Ndani ya Dakika 17

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.