in

Mabadiliko Toleo Jipya la App ya Cheka Point (Android)

Video za kuchekesha kupitia simu yako ya mkononi ya Android

Mabadiliko Toleo Jipya la App ya Cheka Point (Android)

Kama wewe ni mfuatiliaji wa Tanzania Tech basi najua unajua kuwa Tunamiliki app inayoitwa Cheka Point, App hii inaruhusu kupakia video fupi za kuchekesha ambapo pia utapokea Cheka point ambazo unaweza kubadilisha na kuwa salio la kawaida la simu au Pesa taslimu kupitia akaunti zako za M-Pesa na Tigo Pesa.

Hivi karibuni tumeboresha app hiyo na sasa inakuja na muonekano bora na mabadiliko mengi ambayo yatafanya ufurahie siku yako kwa kuangalia video fupi za kuchekesha kupitia simu yako ya Android. Kupitia makala hii tutaenda kuangalia mabadiliko hayo mapya kwenye app ya cheka point.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Video za Wima

Ni wazi kuwa video za wima zimekuwa sehemu ya mitandao mbalimbali siku hizi ndio maana Tanzania Tech kupitia Cheka Point tunakuleta rasmi video za wima. Video hizi zinakuwa kama video za Stories na IGTV ambapo unaweza kuangalia video hizi zikiwa zimejaa kwenye kioo cha simu yako.

Mabadiliko Toleo Jipya la App ya Cheka Point (Android)

Kama unavyoweza kuona sasa utaweza kuona ukurasa wa video za wima kwenye ukurasa wa mwanzo kwenye app, pia utaweza kuna video za wima kwenye kila profile ya mtu ambaye atakuwa na akaunti kwenye app ya Cheka Point. Pale unapo angalia video yoyote ya wima, unaweza ku-swipe kwa kwenda juu na itatokea video nyingine.

Ili kuweka video ya wima huna haja ya kufanya kitu chochote kwani app yenyewe inagundua video ya wima na video ya kawaida, ila kama unataka kuweka video za wima pekee basi hakikisha unaweka video zilizojaa kwa wima, yani zilizopo na size ya stories kwenye au IGTV.

Notification

Sasa utaweza kupokea Notification kila mara mtu atakapo fuata akaunti yako, na pia utaweza kupata notification kila mara mtu huyo anapokuwa anapost Video mpya ya kuchekesha. Pia unaweza kuona video za watu wote ulio wafuata kupitia sehemu ya uliowafuata inayopatikana chini icon ya tatu kutoka upande wa kushoto.

Facebook Login

Kwa sasa mabadiliko mengine ambayo yanaweza yasiwe mazuri kwa kila mtu ni upande wa Facebook Login, awali ndani ya app ulikuwa unaruhusiwa kuingia kwa kutumia Facebook lakini kwa sasa sehemu hiyo imeondolewa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Kwa sasa tuna angalia njia mpya za kuongeza kama vile kuingia kwa kutumia namba za simu ambapo utaweza ku-unganisha akaunti yako ya zamani kupitia namba za simu.

Mabadiliko Toleo Jipya la App ya Cheka Point (Android)

Mabadiliko Mengine

Mabadiliko mengine madogo ni kama vile sasa app inafanya kazi kwa haraka zaidi, ikiwa pamoja na mabadiliko ya icon ambazo sasa zinaonekana zaidi. Pia mfumu mpya wa kutoa maoni ambapo sasa tunapokea maoni yao moja kwa moja.

Hayo ndio baadhi ya mabadiliko kwenye app ya Cheka Point, kama unataka kuona mabadiliko hayo mwenyewe unaweza kupakua app hiyo kupitia soko la Play Store kupitia link hapo chini.

Mabadiliko Toleo Jipya la App ya Cheka Point (Android)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps Muhimu kwaajili ya Mwezi wa Ramadhani (2024)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.