in

Chat Bila Kutumia Internet Kwa Kutumia App Hizi

Hizi hapa app zitakazo kusaidia kuchat bila kutumia internet wala salio

Chat Bila Kutumia Internet Kwa Kutumia App Hizi

Kipindi hichi cha siku kuu najua watu wengi hupenda kujumuika pamoja na ndugu na jamaa ili kuweza kufurahia kwa pamoja sikukuu mbalimbali za mwisho wa mwaka, kuliona hili leo nimekuletea makala ambayo inaweza kukusaidia ku-kuunganisha na ndugu na jamaa kwa kuchat kwa urahisi bila kutumia gharama yoyote zaidi ya simu yako.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha app nzuri ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kuchati na ndugu na jamaa kwa urahisi kabisa bila kutumia Internet wala gharama yoyote, basi bila kupoteza muda zaidi twende nikakuonyeshe app hizi.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Bridgefy

Chat Bila Kutumia Internet Kwa Kutumia App Hizi

Bridgefy ni app nzuri sana ambayo itakusaidia kuchati bila kutumia internet, app hii imejulikana kwa kasi sana kutokana na waandamanaji wa Hong Kong kuitumia app hii kukwepa udhibiti wa mtandao uliowekwa na China. App hii inatumia Bluetooth kuweza kuunganisha mtu mmoja na mwingine na nirahisi sana kutumia na inapatikana bure kabisa kupitia soko la Play Store na App Store.

Bluetooth Chat

Chat Bila Kutumia Internet Kwa Kutumia App Hizi

Bluetooth Chat ni app nyingine nzuri sana ambayo inaweza kukusaidia kuchati na ndugu na jamaa wa karibu bila kutumia internet, app hii ni nzuri sana na inaweza kukusaidia sana hasa kama unataka kuchat na ndugu au jamaa waliopo karibu na wewe. Unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutumia app hii na pia jinsi unavyoweza kuchat na watu wako wa karibu bila kutumia internet wala salio. App hii inapatikana kwa mfumo wa Android pekee.

Bluetooth Chat
Price: Free

FireChat

Chat Bila Kutumia Internet Kwa Kutumia App Hizi

Fire Chat ni app nyingine nzuri sana ambayo itakusaidia kuchat bila kutumia Internet, app hii ni nzuri sana kwani inakusaidia kuchat kwa kutumia Bluetooth na kwa kutumia Wi-Fi hatakama Wi-Fi hiyo haina internet, kitu cha msingi ni kuwa inatakiwa kuwa imeinganishwa kwa mtu zaidi ya mmoja ili kutengeneza network ambayo ndio inaweza kutumiwa na app hii kufikisha meseji na picha mbalimbali kwa urahisi bala kuhitaji internet kabisa.

FireChat
Price: Free

Near Peer

Chat Bila Kutumia Internet Kwa Kutumia App Hizi

Near Peer ni app nyingine nzuri sana ambayo unaweza kutumia kuchat na ndugu na jamaa kwa urahisi bila kutumia internet, app hii ni nzuri sana na inatumia mfumo wa Wi-Fi pekee kuweza kusaidia kuchat kwa urahisi bila kutumia internet, mbali na hayo kitu kizuri kwenye app hii ni kuwa unaweza kutuma meseji kwa mtu na baadae anaweza kupata pale atakapo kuwa karibu, pia unaweza kutengeneza group au ukatumia kuchat kwa mtu mmoja mmoja.

Na hizo ndio app nzuri ambazo unaweza kutumia kuchat na ndugu na jamaa wakaribu bila kutumia internet, kumbuka unaweza kupakua app zote hizi kupitia link china ya maelezo ya app. Kama unataka kujua app nyingine nzuri za kutumia kipindi hichi cha siku kuu basi hakikisha unasoma makala yetu iliyopita ya App nzuri za kujaribu kwenye simu yako ya Android.

Amani Joseph

Chat Bila Kutumia Internet Kwa Kutumia App Hizi

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Namba Mbili Ndani ya Programu Moja ya WhatsApp!

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment