Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy A80

Samsung yazindua simu ya kwanza yenye kamera inyozunguka
Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy A80 Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy A80

Baada ya tamasha la uzinduzi wa simu mpya za Galaxy A kufanyika muda mchache uliopita, hatimaye kupitia mkutano huo kampuni ya Samsung imezindua simu mpya ya Galaxy A80.

Kama ilivyotegemewa Galaxy A80 inakuja na sifa bora sana lakini macho yote hayapo kwenye sifa hizo kwani Galaxy A80 inakuja na kamera za kisasa ambazo ni ngumu kuacha kuziangalia hata kama ukifanikiwa kuona picha tu ya simu hii.

Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy A80Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Samsung Galaxy A80

Advertisement

Kama unavyoweza kuona simu hii inakuja na kamera za kisasa ambazo zina uwezo wa kuzunguka na kuwa kamera za mbele na pia zina uwezo wa kurudi kwa nyuma na kuwa kamera za nyuma, kifupi ni kwamba kamera hizi ndio kamera za mbele na pia ndio kamera za nyuma. Kamera hizo zina uwezo mkubwa kwani ziko kamera za aina tatu tofauti, kamera moja inakuja na Megapixel 48 na nyingine ina Megapixel 8 na ya mwisho ni TOF 3D kamera.

Kamera za simu hii zimetengenezwa maalum kwa ajili ya wale wote wanaopenda kuchukua video za mubashara au (Live Video) ndio maana samsung imeweka kamera hizo zinazo zunguka ambazo zinasemekana kuwa na uwezo mkubwa wa kuchukua video bora kuliko simu yoyote ya Samsung.

Ukiachana na upande wa kamera, Galaxy A80 pia inakuja na sifa nzuri sana kama vile kioo kikubwa cha inch 6.7 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED, kioo hicho pia kinakuja na resolution ya 1080 x 2400 pixel huku kikiwa na sehemu ya fingerprint ambayo ipo chini ya kioo hicho.

Vilevile Galaxy A80 inaendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 730 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 8 pamoja na ukubwa wa ROM wa GB 128. Simu hii haina sehemu ya kuweka Memory card, sifa nyingine za Galaxy A80 ni kama zifuatazo.

https://www.youtube.com/watch?v=GzM1FwLV3Ds

Sifa za Samsung Galaxy A80

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.7 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2400 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie) yenye mfumo wa One UI
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz Kryo 460 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 460 Silver).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM730 Snapdragon 730 (8 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 618
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128 huku zote ikiwa na Haina uwezo wa kuongezewa na memory card.
  • Ukubwa wa RAM –  GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Kamera za mbele ndio hizo hizo kamera za nyuma.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/2.0, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 yenye f/2.2 f/2.2, 12mm (ultrawide) na kamera ya mwisho ni TOF 3D kamera. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-ion 3700 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0 na GPS ya A-GPS, GLONASS. USB ya microUSB 2.0, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi tatu za Angel Gold, Ghost White, Phantom Black.
  • Mengineyo – Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, gyro, proximity na compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G.
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Bei ya Samsung Galaxy A80

Kwa upande wa bei ya Galaxy A80, kwa mujibu wa tovuti ya Sammobile simu hii itaanza kupatikana kuanzia tarehe 29 mwezi wa tano mwaka huu na inategemea kuuzwa kwa Euro € 649 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Tanzania Tsh 1,690,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use