in

WhatsApp Kuonyesha Mara Ngapi Meseji Yako Imeforwardiwa

Sasa utaweza kujua idadi ya watu walio forward meseji hadi kukufikia wewe

WhatsApp Kuonyesha Mara Ngapi Meseji Yako Imeforwardiwa

Siku za karibuni tulipata ripoti kuwa WhatsApp inakuja na njia ya kuweza kujua picha feki, lakini kama hiyo haitoshi siku za karibuni ripoti mpya zimeibuka kuhusu ujio wa sehemu mpya ambayo itakuwezesha kujua idadi ya watu ambao wame-forward meseji uliyo tumiwa na watu wengine.

WhatsApp Kuonyesha Mara Ngapi Meseji Yako Imeforwardiwa

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Sehemu hii itaonekana endapo meseji hiyo ime-forwardiwa na mtu mwingine na wewe ume-forward meseji hiyo kwa mtu mwingine, baada ya hapo utabofya sehemu ya info na hapo utaona idadi ya meseji hiyo imeforwardiwa na watu wangapi hadi kufikia kwako.

Mbali na sehemu hiyo, inasemekana kuwa kuna sehemu nyingine ambayo itakuwa inaonyesha kama meseji imeforwardiwa mara nyingi. Sehemu hiyo inaitwa “Frequently forwarded” hii itakuwa juu ya meseji iliyo forwardiwa zaidi ya mara tano.

WhatsApp Kuonyesha Mara Ngapi Meseji Yako Imeforwardiwa

Hata hivyo inasemekana kuwa sehemu ya kuangalia idadi ya watu walio forward meseji haitoweza kuonekana kama meseji hiyo ime-forwardiwa zaidi ya mara 5. Kwa sasa sehemu hizi zinapatikana kwenye programu ya majaribio ya WhatsApp Beta, hivyo inasemekana sehemu hizi zitakuja kwenye programu ya WhatsApp ya Android kabla ya programu ya iOS.

Amani Joseph

WhatsApp Kuonyesha Mara Ngapi Meseji Yako Imeforwardiwa

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps Nzuri Kwaajili ya Kupakua Video za Aina Yoyote

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments