in

NASA Inalipa Milioni 42 Kwa Kazi ya Kulala Kitandani Miezi 2

Ndani ya miezi yote hiyo mtu atakuwa amelala bila kusimama wala kukaa

NASA Inalipa Milioni 42 Kwa Kazi ya Kulala Kitandani Miezi 2

Karibu kwenye makala nyingine ya Je wajua tech na leo tunaenda kuangalia swala la PESA ambalo najua wengi wetu tunapenda kujua. Sasa mara nyingi kwenye kipengele hichi hua tunaongelea maswala yaliyopita kidogo lakini hili la leo halina hata wiki moja toka kutangazwa.

Kwa kifupi ni kwamba, Shirika linalo jihusisha na utafiti wa anga marekani NASA hivi karibuni ilitangaza kulipa kiasi cha Euro £14,000 ambayo ni sawa na takribani zaidi ya Shilingi za kitanzania Tsh Milioni 42, kwa mtu yeyote atakaye weza kulala kitandani kwa miezi miwili…rahisi ehh.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa mujibu wa tovuti ya The independent, inasemekana kuwa hatua hii itawasaidia watafiti kutoka shirika hilo kuweza kutambua jinsi kani ya mvutano au Graviti ya kutengeneza inavyoweza kuadhiri mwili wa binadamu. Kwa kupitia utafiti huo uliopewa jina la AGBRESA au (Artificial Gravity Bed Rest Study) wanasayansi wataweza kujua matumizi ya kani ya mvutano ya kutengeneza ili kuzuia madhara ya kutokuwa na uzito wanapo kuwa kwenye utafiti wa anga.

Sasa inasemekana wanatakiwa watu 24 ambapo 12 wanatakiwa kuwa wanawake na 12 wanatakiwa kuwa Wanaume. Watu wote watakao shiriki wanatakiwa kuwa na umri kati ya miaka 24 mpaka miaka 55 na wanatakiwa wawe wanaongea kijerumani kwa sababu utafiti huu unafanyika huko ujerumani.

Uchunguzi wenyewe utahusisha watu wote kulala kwenye kitanda kwa muda wa siku 60 na ndani ya kipindi chote hicho watu wote hawato ruhusiwa kutembea wala kukaa, shughuli zote za chakula pamoja na mapumziko zitafanyika wakati mtu akiwa amelala. Kama ukiamua kushiriki, NASA imesema kuwa mtu unatakiwa kukaa kwenye eneo hilo la utafiti kwa jumla ya siku 89, hii ikiwa pamoja na siku 14 za kuzoea mazingira pamoja na siku hizo 60 za kulala kitandani.

Wakati wa utafiti inasemekana watu walio chaguliwa watalala kwenye vitanda ambavyo vitakuwa na uwezo wa kuzunguka kwa kasi ambapo hii ni sawa na mazoezi wanayo pitia wataalamu wa anga kutoka kwenye shirika hilo.

NASA Inalipa Milioni 42 Kwa Kazi ya Kulala Kitandani Miezi 2

Kama unavyoweza kuona hapo juu hivyo ndivyo kitanda hicho kitakavyokuwa na upande wa kushoto chini ndipo mtu atakapokuwa analala kwa muda wote wa uchunguzi huo. Vilevile hivi ndivyo itakavyokuwa kwenye muda wa mapumziko ambapo hapo ndipo washiriki watapewa chakula na huduma nyingine ikiwa pamoja na kuangaliwa kiafya kabla ya kuendelea na utafiti.

NASA Inalipa Milioni 42 Kwa Kazi ya Kulala Kitandani Miezi 2

Picha hapo juu inaonyesha jinsi muda wa utafiti itakavyokuwa na jinsi kitanda hicho kitakapo kuwa kinazungushwa kwa kasi ili kuangalia matokeo hayo ya kani ya uvutano ya kutengeneza ambayo itawasaidia wanasayansi wa NASA kuweza kuitumia kwenye kuepuka adhari za kutokuwa na uzito ( weightlessness ) wanapokuwa kwenye tafiti zao nje ya dunia.

Kama kwa namna yoyote uko ujerumani au unaweza kuongea kijerumani basi inasemekana hadi sasa bado milango ipo wazi kutafuta watu hawa na kama unataka ku-appy kwa mujibu wa independent unaweza kutuma barua pepe ya maombi kupitia probanden-bit@dlr.de

Je unaonaje hii, unadhani unaweza kufanya kitu kama hichi kwaajili tu ya kujizolea zaidi ya Tsh milioni 42 za kitanzania.? Tuambie kwenye maoni hapo chini. Kwa makala zaidi za je wajua unaweza kusoma hapa kujua jinsi mabaki ya simu yanavyotumika kutengeneza medali za Olympics 2020, pia usiache kutembelea Tanzania Tech kila siku ili kupata habari mpya za Teknolojia.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments