in

Jiandae na Nokia 9 Simu ya Kwanza Yenye Kamera (5) Tano

Hii ndio itakuwa Simu ya kwanza ya Nokia yenye kamera (5) tano kwa nyuma

Nokia 9

Kampuni ya Nokia inajiandaa kuanza mwaka 2019 kwa namna ya kipekee, kama inavyo tabiriwa mwaka 2019 utakuwa ni mwaka wa simu nyingi kuwa na kamera zaidi ya mbili kwa nyuma. Ndio maana kampuni ya Nokia nayo inajiandaa kuja na simu yake mpya ya Nokia 9, ambayo inasemekana kuja na kamera 5 kwa nyuma.

Nokia 9 View

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kwa mujibu wa tetesi mbalimbali mtandaoni Nokia 9 inatarajiwa kuzinduliwa mapema mwishoni mwa mwezi wa kwanza kupitia CES 2019, mkutano ambao hutumiwa na makampuni mbalimbali kuonyesha teknolojia mpya.

Mbali na hayo Nokia 9 inatarajiwa kuwa simu ya kwanza kutoka kampuni hiyo kuwa na idadi kubwa ya kamera huku ikisemekana kuja na kamera 5 kwa nyuma pamoja na kamera ya selfie ambayo inasemekana kuja na Megapixel 12. Tetesi hizo pia zinadai kuwa Nokia 9 itakujua na processor ya Snapdragon 845 chipset ambayo itakuwa inasaidiwa na RAM ya GB 8 pamoja na ukubwa wa ndani wa hadi GB 128.

nokia-9

Simu hii pia inatarajiwa kuja na battery kubwa yenye uwezo wa 4,150 mAh battery ambayo pia itakuja na teknolojia ya Fast Charging. Mengine kuhusu simu hii ni pamoja na uwezo wa kuzuia maji na vumbi (IP68 dust/water proof), kioo cha AMOLED ambacho kitakuwa na ulinzi wa Corning Gorilla Glass.

Kwa sasa tuendelee kusubiri simu hii mpya ya Nokia 9, pamoja na simu nyingine kutoka makampuni mengine kama Samsung ambayo nayo inatarajia kuja na simu nyingine zenye uwezo wa kamera zaidi ya mbili, ikiwa pamoja na ile ambayo inasemekana kuja na uwezo wa hadi kamera tisa kwa nyuma.

Amani Joseph

Jiandae na Nokia 9 Simu ya Kwanza Yenye Kamera (5) Tano

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apple Yathibitisha iPhone 15 Kuzinduliwa 12 Septemba

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment