in

Instagram Yaongeza Kipengele cha Shopping Kwenye Stories

Sasa utaweza kununua bidhaa kupitia Tab Maalum ya Shopping kupitia Instagram

instagram shopping

Wakati mtandao wa Instagram ukiwa kwenye hatua za awali za kuja na programu maalum ya kununua bidhaa kwa kupitia akaunti za Instagram, Kampuni ya Facebook kupitia mtandao wa huo wa Instagram hivi leo imetangaza kuja na njia mpya ya kuweza kurahisha watu kununua bidhaa moja kwa moja kupitia kwenye app ya Instagram.

Kupitia sehemu ya Stories, Instagram inategemea kuleta sehemu mpya ya Shopping ambayo itakuwa kwenye sehemu ya Explore iliyotambulishwa hivi karibuni ambapo Kupitia sehemu hiyo ya Stories utaweza kuona bidhaa mbalimbali zikiwa zimewekewa stika ambazo utakapo bofya hapo utapelekwa moja kwa moja kwenye tovuti yenye bidhaa uliyo iona kupitia sehemu hiyo ya Stories.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kama unavyoweza kuona sehemu hiyo kwenye picha hapo juu, pale utakapo bofya sehemu ya Shopping Explore utaweza kuona bidhaa nyingi kutoka kwenye akaunti mbalimbali ndani ya mtandao wa Instagram. Mbali ya hayo pia watumiaji wa mtandao huo watapewa uwezo wa kuuza bidhaa mbalimbali kwa urahisi kwa kuweka stika ya Shopping ambayo itapatikana kwenye sehemu ya Stika kwenye sehemu ya Stories.

Sehemu hii inatarajiwa kuwafikia watumiaji mbalimbali kuanzia siku ya leo hivyo hakikisha unasasisha (update) toleo jipya la App ya Instagram kupitia masoko ya Play Store na App Store.

Apps Nzuri Kwa Simu za Android Zilizopo Rooted

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.