in

Hii Hapa Simu ya Kwanza Yenye Ukubwa wa Ndani wa GB 1000

Simu hii inakuja na ukubwa wa ndani wa Terabyte 1 (TB 1)

Simu ya Smartisan R1

Ikiwa bado kampuni nyingi za simu zina tengeneza simu zenye ukubwa wa ndani wa GB 16 hadi GB 256, hivi karibuni imekuja simu ya kwanza yenye kubadilisha mtazamo wa kampuni nyingi za Simu hasa kwenye upande wa ukubwa wa ndani. Smartisan R1 hilo ndio jina la simu iliyovunja rekodi mwaka huu 2018 kwa kuwa simu yenye ukubwa wa ndani mkubwa zaidi, simu hii inakuja na ukubwa wa ndani wa GB 1000 sawa na Terabyte 1.

Mbali na hayo simu hii inakuja na processor ya Snapdragon 845 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 8. Simu hii pia inakuja na machaguo mengine ambayo yenyewe yanakuja na ukubwa wa ndani wa GB 64 na GB 128 ambayo yenyewe yanakuja na uwezo wa RAM ya GB 6 na GB 8.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Simu hii pia inakuja na kamera ya mbele yenye uwezo wa Megapixel 24 yenye uwezo wa f/2.0, na kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 12 yenye f/1.8 na nyingine ikiwa na uwezo wa Megapixel 20 yenye f/1.75. Simu hii ya Smartisan R1 inakuja na battery ya 3,600 mAh battery yenye uwezo wa teknolojia ya Qualcomm’s Quick Charge 4+ yenye uwezo wa kujaza battery ya simu hiyo kwa haraka zaidi.

Simu hizi zitapatikana kwa nchini china na bei zake zitakuwa kama ifuatavyo, Smartisan R1 ya RAM ya GB 6 na ukubwa wa GB 64 itauzwa kwa Yuan ya china CNY3,499 ($549) sawa na Tsh 1,253,000. Kwa simu ya Smartisan R1 yenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ndani wa GB 128 itauzwa kwa Yuan CNY3,999 ($627) sawa na Tsh 1,431,000 na Simu ya Smartisan R1 yenye RAM ya 8 na ukubwa wa ndani wa 1TB itauzwa kwa Yuan ya china CNY8,848 ($1388) sawa na Tsh 3,168,000. Simu hii inapatikana kwa nchini china tu kwa sasa.

Kampuni ya Nokia Kubadilisha Logo Yake ya "NOKIA"

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment