in

Samsung Yazindua Laptop Mpya za Notebook 5 na Notebook 3

Laptop hizi ni bei nafuu zaidi ya laptop za Notebook 7 Spin na Notebook 9

Laptop mpya za Samsung Notebook 5 na Notebook 3

Kampuni ya Samsung imetangaza kupitia ukurasa wake wa habari kuwa, imetoa laptop mpya mbili ambazo zitakuwa ni muondelezo wa matoleo ya laptop za Samsung Notebook 5 pamoja na Notebook 3. Laptop hizo mbili zinakuja zikiwa na bei nafuu zaidi ya zile ambazo ziko sokoni za Notebook 7 Spin pamoja na Notebook 9 models.

Laptop hizi za sasa zinasemekana kuja zikiwa zimeboreshwa zaidi pamoja na sifa mpya huku zikiwa na muonekano wa kisasa zaidi. Habari kutoka kwenye tovuti ya Samsung zinasema laptop ya Notebook 3 inakuja kwa aina mbili yaani laptop yenye kioo cha inch 14 na nyingine ikiwa na nchi 15, sifa zingine za laptop hizi ni kama zifuatazo –

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot

Sifa za Laptop ya Samsung Notebook 3

Samsung Notebook 3 Inch 14

 • Processor – 8th Generation Intel KBL-RU Quad Core au 7th Generation Intel KBL-U Dual Core
 • Display – HD Resolution
 • Memory – DDR4
 • Storage – SSD + HDD
 • Network – ac1x1 LAN (10/100)
 • Graphics – Shared NVIDIA MX110 (2GB Memory)
 • Battery – 43Wh
 • Camera – VGA
 • Colors – Misty Gray, Night Charcoal, Deep Peach
 • Dimension – 336.0 x 232.9 x 19.8 mm
 • Weight – 1.66kg

Samsung Notebook 3 Inch 15

 • Processor – Quad Core 7th Generation Intel KBL-U Dual Core
 • Display – Full HD Resolution ¦ HD Resolution
 • Memory – DDR4
 • Storage – SSD + HDD
 • Network – ac1x1 LAN (10/100)
 • Graphics – Shared NVIDIA MX110 (2GB Memory)
 • Battery – 43Wh
 • Camera – VGA
 • Colors – Misty Gray, Night Charcoal, Deep Peach, Pure White
 • Dimension – 377.4 x 248.6 x 19.6 mm
 • Weight – 1.97kg

Kuhusu bei Laptop hizi bado hazija tangazwa bei zake lakini inasemekana zitakuja zikiwa na bei nafuu kuliko zile zilizopo sokoni kwa sasa. Kwa upande wa ukubwa wa hard disk pia samsung haijaweka wazi ukubwa wake bali zaidi wamesema laptop hizo zitakuja zikiwa na hard disk za aina zote yaani SSD pamoja na HDD.

Sifa za Laptop ya Notebook 5

Samsung Notebook 515” Display
Processor8th Generation Intel KBL-RU Quad Core ¦7th Generation Intel KBL U
Display15.6” Full HD (Wide Viewing)
MemoryDDR4
StorageSSD + HDD
Networkac1x1 LAN (10/100)
GraphicsShared¦NVIDIA MX150 GDDR5 2G
Battery43Wh
CameraVGA
ColorsLight Titan
Height377.4 x 248.6 x 19.9 mm
Weight1.97kg

Laptop hizi zote zinategemewa kuanza kupatikana kwenye robo ya pili ya mwaka ambapo ni kuanzia mwezi wa April 1, 2018 hadi June 30, 2018. Hata hivyo laptop hizi zitaanza kupatikana kwa nchi za Korea na baadae kufuatiwa na nchi za China, Brazil na baadae nchi zingine.

Laptop za Mwaka 2021 Ambazo ni Bora Kwa Matumizi 2023

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment