in

Google Yaja na Song Maker Njia Rahisi ya Kutengeneza Muziki

Sasa tengeneza muziki kupitia simu yako ya mkononi

Kutengeneza Muziki na Song Maker

Google kupitia idara yake ya muziki inayo julikana kama Chrome Music Lab, mwaka huu 2018 imezindua Song Maker njia nyingine rahisi ya kutengeneza muziki kupitia kifaa chako iwe ni simu, kompyuta au hata tablet njia hii ni rahisi kutumia na inafurahisha na unaweza kutengeneza muziki bora.

Song Maker hufanya kazi kama ifuatavyo, unachotakiwa kufanya ni kuweka alama za rangi kwenye kila kichumba kwa mpangilio fulani, huku pia ukiweza kubadilisha ala za muziki mbalimbali na baadae muziki utaweza kuundwa bila hata wewe kuingia studio au kutumia kazi kubwa. Kizuri ni kuwa unaweza kushiriki ulicho tengeneza na mtu yoyote na haya yote yanafanyika bila ku-login au kutengeneza akaunti yoyote.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Unaweza kuanza kutengeneza muziki wako kwa kuingia kwenye tovuti hapo chini kisha tengeneza muziki unao upenda kisha shiriki na marafiki zako, pengine hii itakusaidia utakuwa umepata njia rahisi ya kufanya mazoezi ya muziki na kukusaidia kufanikiwa kimuziki.

BOFYA HAPA KUTENGENEZA MUZIKI

Mtandao wa Twitter Kubadilishwa na Kuwa "X"

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.