in

Picha za Simu Mpya Zinazokuja za Nokia 7 Plus na Nokia 1

Simu hizi zitakuja zikiwa na mfumo rahisi wa Android One

Picha za Simu Mpya Zinazokuja za Nokia 7 Plus na Nokia 1

Hivi karibuni kampuni ya Nokia kupitia muwakilishi wake HDM Global imefanikiwa kutoa simu mbalimbali za Nokia Android ambazo zimeuza mamilioni ya Nakala dunia nzima na kuzishinda kampuni kama HTC, Sony, Google, Lenovo na kampuni zingine zenye kutoa simu zinazotumia mfumo wa Android.

Lakini kama haitoshi kampuni ya Nokia inajiandaa kurudi na simu zake mpya za Nokia 7 Plus pamoja na Nokia 1 simu hizi zote zinategemewa kuzinduliwa kwenye mkutano wa Mobile World Congress (MWC) ambao unategemewa kuanza hivi karibuni huko nchini Barcelona.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kupitia akaunti ya twitter ya mvujishaji maarufu Evan Blass, tumefanikiwa kupata picha ya simu hizo kabla ya kutoka kwake.

Nokia 1 inasemekana kuwa simu ya bei rahisi sana huku ikiwa na mfumo wa uendeshaji mwepesi wa Android One, ambao ni maalum kwaajili ya simu zenye uwezo mdogo wa RAM (kuanzia MB 512 hadi GB 1) pamoja na uwezo mdogo wa ukubwa wa ndani (kuanzia GB 1 hadi GB 8).

Kwa upande wa Nokia 7 Plus hii inategemewa pia kuja na mfumo wa uendeshaji wa Android One. huku ikiwa na uwezo wa processor ya Snapdragon 660 kioo cha inch 18:9 pamoja na RAM ya GB 4 huku ikisaidiwa na ukubwa wa ndani wa GB 64.

Kwa sasa bado hakuna sifa zaidi za simu hizi, lakini tuna ahidi kukuletea habari zaidi pindi tutakapo pata habari zaidi ikiwa pamoja na sifa kamili za simu hizi za Nokia 7 Plus pamoja na Nokia 1.

Google Kuzindua Simu Mpya za Pixel 8 Mwezi Oktoba (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments

  1. Maoni* mkazi wa masumbwe mbogwe geita mwanza tanzania niko kakola. napenda kusema kua simu ya nokia nisimu inayotegemewa na wengi kawaida wange changanya tach na singolain sababu wapo hawapendi kutumia tach au dambo laini ambayo ni simu ya batani kwahiyo mchango wangu ni huo tu?