in

Hizi Hapa Ndio Laptop Ngumu Zaidi kwa Mwaka 2018

Laptop hizi zinaweza kuhimili vumbi, joto, baridi na hata maji

Laptop Ngumu 2018

Wote tunapenda laptop zenye sifa nzuri, lakini ni watu wachache sana wanapenda laptop zenye sifa za kuwa laptop ngumu zaidi. Sasa baada ya kufanya utafiti nimekuletea list hii ya Laptop ngumu zaidi kwa mwaka 2017 – 2018.

1. Panasonic Toughbook

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Panasonic Toughbook ni moja kati ya laptop ngumu sana mpaka sasa, mbali na kuwa ngumu laptop hii ina ubora wa hali ya juu ikiwa na uwezo wa kuzuia maji uwezo wa kuzuia vumbi mchanga na hata uwezo wa kuhimili baridi kali.

2. Dell Latitude 7212 Rugged Extreme

Tofauti na latop ya Panasonic kompyuta ya Dell Latitude 7212 Rugged Extreme, hii iko kwa mfumo wa tablet na pamoja na kuwa iko kwenye mfumo huo ambao ni wa kioo kitupu lakini bado hii ni moja kati ya kompyuta, tablet ngumu zaidi mpaka sasa.

3. HP Probook x360

Tofauti na laptop nyingine kwenye list hii laptop ya HP Probook x360 ni latop ambayo imetengenezwa kawaida sana kama laptop nyingine, lakini tofauti ya kompyuta hii imetengenezwa kwa ajili ya wanafunzi na ni moja kati ya laptop ngumu sana kwa aina hii. Laptop hii inaweza kuhimili maji, vumbi kuanguka na mambo mengine.

4. Lenovo ThinkPad T450S

Laptop hii ya Lenovo ThinkPad T450S nayo ni moja kati ya laptop ngumu zaidi na tofauti na laptop nyingine laptop hii ni ngumu kiasi kwamba hata kama ukifanikiwa kuharibu uso wake bado sakiti ya laptop hiyo itaendelea kufanya kazi.

Na hizo ndio baadhi tu ya laptop ambazo ni ngumu na kutokana na majaribio yalio fanywa na baadhi ya kampuni basi zimefanikiwa kushika taji la laptop ngumu zaidi. Je vipi unadhani kati ya hizi ni laptop gani ambayo ni ngumu zaidi kuliko nyingine..?

Kama unataka kujua list ya laptop bora ambazo unaweza kununua kwaajili ya wanafunzi unaweza kusoma hapa list ya laptop bora za kununua mwaka huu kwaajili ya wanafunzi.

China Kuanzisha Mfuko wa Kusaidia Utengenezaji wa "Chipset"

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments