in

Apple Yatoa Mfumo Mpya wa iOS 11.1 (Download Sasa Hapa)

Unaweza kuinstall upya toleo hili kwa kutumia link hapo chini

iOS-11.1

Kama kawaida leo Apple imetangaza mfumo wake mpya wa iOS 11.1 mfumo huu sasa unakuja na maboresho mengi. Maboresho yanayo onekana kwa haraka ni pamoja na ujio wa emoji nyingi mpya pamoja na kurudi kwa App ya 3D Touch app switcher gesture.

Kama unataka ku-update toleo jipya kupitia kifaa chako basi ni vyema kufuata hatua hizi ambazo zitaweza kuelekeza jinsi ya kufanya hivyo. Muhimu kumbuka kuchaji kifaa chako hadi asilimia 50 kabla ya kuanza ku-update, vilevile hakikisha una bando la kutosha angalau GB 1 au zaidi au inaweza kuwa zaidi kutokana na kifaa unachotumia.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Kwa kuanza ingia kwenye Settings.
  • Alafu bofya General > Software Update.
  • Subiri kidogo wakati ukurasa huo ukitafuta update kumbuka inaweza kuchukua muda kidogo.
  • Baada ya update kuonekana bofya Download and Install.
  • Kisha update zitaangaliwa na Apple kisha zitawekwa kwenye kifaa chako.

Lakini kama unataka ku-update kifaa chako kwa toleo hili jipya kwa kutumia programu ya iTunes basi unaweza kupata link za kudownload mafile maalum kulingana na simu yako, kumbuka kuchagua link yenye jina la kifaa chako.

Download iOS 11.1 IPSW Files

Kama unataka msaada zaidi unaweza kutuandikia kwenye maoni hapo chini. Kwa habari zaidi za teknolojia usisahau kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play Store nasi tutakujuza habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.

Apps za Kurahisisha Matumizi ya Mtandao wa Instagram

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.