in

Sababu Kwanini Smartphone Yako Inaisha Chaji Haraka

Kama simu yako inaisha chaji haraka, basi soma hii ni kwaajili yako!

Simu kuisha chaji Haraka

Kwa namna moja ama nyingine lazima ulisha wahi kujiuliza hili swali, pengine ni kutokana na simu yako kuto dumu na chaji kwa muda unaotakiwa na pengine ni kutokana na kushindwa kutumia simu yako kila mara kama ulivyo taka, kukusaidi kwenye hili leo ninakupa sababu kwanini simu yako hiyo inaisha chaji mara kwa mara na haraka kuliko unavyotarajia. so lets get to it…

Kushindwa Kuchaji Simu Vizuri

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot

Sababu hii ni ya msingi sana na ndio maana nimeiweka ya kwanza kabisa, wengi wetu hatujui kuchaji smartphone zetu pamoja na kwamba tumekua tukizitumia simu hizo kwa muda sasa. kusaidia kwenye hilo hizi hapa ndio hatua za kuchaji simu yako vizuri na hizi hapa ndio njia za kuchaji simu yako vizuri ili iweze kudumu na chaji.

 1. Kwanza hakikisha unachaji simu yako pale inapofikia asilimia 10 au 15 kwani simu inapo isha chaji kabisa ndipo inapo weza kujaa chaji vizuri na kudumu na chaji kwa muda unaotakiwa.
 2. Pili jitahidi unapochaji simu yako weka flight mode au zima kabisa simu yako ila ni vizuri zaidi kama ungeweza kuweka flight mode kwa kuwa simu inajaa chaji vizuri ikiwa imewaka lakini haitumiki.
 3. Hakikisha battery ya simu yako imebana vizuri kwenye koili za chaji za simu yako kwani kuna kiwango kikubwa sana cha chaji kinapotea kama simu yako imelega lega kugusana vizuri na koili zinazotumika kuchaji simu yako.
 4. Tumia chaji sahihi kuchaji simu yako pia kumbuka kuangalia volt zinazo itajika kuchaji simu yako na hakikisha chaji hiyo imeshika vizuri (imebana) kwenye simu yako.
 5. Pale simu yako inapo jaa chaji usitoe haraka haraka bali subiri angalau nusu saa au dakika ishirini ili simu yako iweze kujaa vizuri.

Kutumia Programu Zenye Mtangazo Mengi

Sababu nyingine inayo sababisha kufanya simu yako kuisha chaji kwa haraka ni kutumia programu zenye matangazo mengi ni kivipi basi hizi hapoa ndio sababu. Ukweli ni kwamba kwenye majaribio mbalimbali yaliyofanywa na wataalamu wa mitandao yamebaini kuwa programu zenye matangazo mengi uchukua karibia asilimia 30 ya chaji kwenye simu yako, hivyo kwa kuwa na programu hizo elewa kuwa simu yako inapojaa chaji toa asilimia 30 ambazo zitatumiwa na programu hizo na hapo utakuwa umebakiwa na chaji asilimia 70 hivyo utaona simu yako imeisha chaji kwa haraka kumbe ni programu zako unazoumia.

Kuchaji Simu Kila Mara au Kutumia Power Bank

Kumesha kuwa na kesi nyingi sana za watu kulala mika mara baada ya kutumia power bank basi simu imekua haidumu na chaji hii usababishwa na tofauti na kuchaji kwenye umeme kuchaji battery kwa kutumia battery ni mfumo ambao umesemekana sio mzuri unatoa kiasi cha umeme ambacho ni hafifu na kufanya battery ya simu yako kushindwa kuimili chaji ya umeme wa soketi hivyo kutokudumu na chaji. Vile vile kuchaji kila saa simu yako kunafanya battery ya simu yako kuzidiwa na kufanya battery yako kuchoka haraka na kushindwa kuimili chaji kwa muda kama ilivyokuwa hapo hawali.

Kuchaji Simu Kwenye Mazingira ya Joto Sana au Baridi Sana

Kuchaji simu kwenye mazingira ya joto sana au baridi sana kunafanya simu yako kuchaji kwa haraka sana au taratibu sana hivyo kupelekea battery yako kutokupata chaji vizuri na kusababisha simu yako kuisha chaji kwa haraka.

Kwa kuzingatia haya na mengine ambayo tayari unayajua utaweza kufanya simu yako kuacha tabia ya kuisha chaji kwa haraka. Pia kama unatumia mfumo wa iOS unaweza ukapitia njia za kufanya simu yako kudumu na chaji hapa.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video. 

Fahamu Hili Kabla ya Kununua Simu Yoyote ya iPhone

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

11 Comments

  • Kuna sababu nyingi sana zinazo sababisha simu kupata joto, sababu moja ya kawaida ni kutumia simu yako kwa muda mrefu kwa mfano, kama unacheza game kwenye simu yako kila mara basi lazima simu yako itakuwa inapata moto. Unaweza kupunguza matumizi makubwa ya simu yako ili kuanza kufanya utafiti wa kujua tatizo.