in

YouTube Inakuja na Mtindo Mpya na Hivi Ndivyo Jinsi ya Kujaribu

Hivi karibuni Youtube inategemea kuja na mtindo mpya na hivi ndivyo ulivyo

Mtindo Mpya Youtube
PICHA THENEXTWEB

Kampuni ya Google kupitia mtandao wake wa youtube hivi karibuni imetangaza kuleta mtindo mpya wa mtandao wake maarufu wa Youtube, mtindo huo mpya ambao utakuwa na uwezo zaidi wa kufanya mtandao huo kutumika kirahisi na kwa haraka zaidi unategemewa kuanza kutumiaka hivi karibuni wakati sasa ukiwa kwenye hatua za majaribio.

Wakati kwa sasa ukiwa bado ujaweza kuona mtindo huo mpya Youtube wanakualika kuweza kujaribu mtindo huo mpya ambao umebadilika sana na wenye sehemu mpya kama vile Dark Theme sehemu itakayo kuwezesha kuondoa rangi nyeupe na kuweka nyeusi ili kulinda macho yako hasa wakati wa usiku. Mtindo huu mpya pia unakuja na sehemu ya Restricted Mode sehemu itakayo kupa uwezo wa kuficha video ambazo unaona hazifai kuonekana na jamii au watoto wadogo.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Mtindo huo mpya kwa sasa huko kwenye hatua za mwisho na bado unaendelea kuboreshwa zaidi hivyo unaweza kuona sehemu mpya zaidi pale mfumo huo utakapo kamilika, kama unapendelea kuwa wa kwanza kujaribu mtindo huo mpya unaweza kubofya hapa Youtube New kisha bofya Try it Now ili kujaribu mtindo huo moja kwa moja kabla ya kutoka kwake rasmi.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Infinix Yashinda Tuzo za Design Kimataifa (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.