in

Kutana na Jelly Simu Ndogo ya Android yenye Inch 2.45 na 4G

Kutana na simu Android ambayo pengine ni ndogo kuliko zote duniani

Kutana na Jelly Simu Ndogo ya Android yenye Inch 2.45 na 4G

Wakati simu zikiwa zinaendelea kutoka kila siku na ubora wa simu hizo kupimwa kwa ukubwa wa kioo, huko Shanghai kampuni moja inayo chipukia inayoitwa Unihertz imefanikiwa kutengeneza smartphone ndogo kuliko zote yenye uwezo wa 4G.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Simu hiyo ambayo ambayo ina uwezo wa kuenea kwenye mfuko wako mdogo wa jensi imetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa huku ikiwa na processor ya GHz 1.1 RAM ya 2GB pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 16, uwezo wa memory haujaishia hapo kwani simu hii inaweza kuongezewa memory kwa kutumia memory card ya mpaka GB 32. Kwa upande wa camera simu hii inayo kamera ya nyuma ya mega pixel 8 pamoja na kamera ya mbele ya mega pixel 2.

Kwa upande wa kioo simu hii ina kioo cha 240 x 432 pixels pamoja na uwezo wa battery wa 950mAh ambapo inaweza kudumu na chaji kwa siku tatu na kuendelea kwa matumizi ya kawaida, kikubwa zaidi simu hii inatumia toleo jipya kabisa la Android 7 ambalo linapatika kwenye simu chache sana kwa sasa. Lakini kingine kuhusu jelly ni bei yake, simu hii inauzwa itauzwa kwa dollar za marekani $59 sawa na shilingi za Tanzania 132,000 kwa toleo la kawaida na dollar $75 sawa na shilingi za Tanzania 170,000 kwa toleo la pro.

Simu hii kwa sasa iko kwenye hatua za awali sana ili kuanza kuuzwa kote dunia, hivyo itakubidi kuwa mvumilivu kusubiri kidogo mpaka simu hii ya jelly itakapo kufikia hasa kwenye maduka ya hapa Tanzania.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Zifahamu Apple Watch Series 9 pamoja na Watch Ultra 2

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.