in

Sasa Matangazo YouTube ni Kwa Channel Zenye Views 10k Pekee

Sasa hutoweza kuonyesha matangazo kwenye akaunti yako kama huna views 10,000

Sasa Matangazo YouTube ni Kwa Channel Zenye Views 10k Pekee

Kampuni ya Google kupitia mtandao wake wa YouTube mapema leo imetangaza utaratibu mpya ambapo sasa hutoweza kuonyesha matangazo kwenye channel yako kama channel yako haijafikisha views elfu kumi (10,000) na kuendelea.

Kwa mujibu wa post iliyoko kwenye blog ya Youtube utaratibu huo mpya umekuja baada ya ongezeko la channel au akaunti zenye kuiba video kutoka channel zingine kwa lengo la kujipatia kipato kwa haraka. Hata hivyo sheria hiyo imekuja wakati kampuni hiyo ikiwa kwenye kipindi kigumu kutokana na kupata hasara kubwa baada ya baadhi ya makampuni makubwa ambayo hufanya matangazo kupitia mtandao huo kujitoa kwa kile kinacho semekana kuwa matangazo yao huonyeshwa kwenye video zisizo na maadili na zenye kuvunja haki za binadamu.

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot

Hivyo basi kuanzia wiki ijayo kati ya Jumatano na Alhamisi channel zote za YouTube zenye views chini ya elfu kumi (10,000) zita ondolewa matangazo mpaka hapo zitakapo fikia kiwango hicho cha views, YouTube huwa inahesabu views moja (1) kila baada ya mtu anapo angalia video kwa muda wa sekunde zaidi ya thelathini (30). Vilevile YouTube imetangaza kuboresha zaidi sheria zake za (YouTube Partner Program) pale unapokuwa unaomba matangazo hivyo sasa channel yako itabidi kupitiwa kwanza mara kadhaa kabla ya kuruhusiwa kuonyesha matangazo.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

Jinsi ya Kutumia Google Bard, Mfumo wa AI Kama ChatGPT

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

12 Comments

 1. Me nataka unisaidie wasitani wakulipwa viaws nikuanzia ngapy naomb ?? nisaidie•

  mana kunamt kanifungulia account afu akaniambia was tan wakulipwa viaws nikuanzia 1000•

  Zimefika 1000 akaniambia tena zikifika 4000 unitafute nikuunganishie uanze kulipwa naomba nisaidie kwailo

  Kwasababu yeye ndo alienifungulia accaunt

  • Hapo sina uhakika na swali ulilo uliza bali, nadhani una maana ya kiwango cha view ambacho unatakiwa kuanza kuonyesha matangazo. Kwa kawaida unatakiwa kufikisha views zaidi ya 10,000 na subscriber 1000. Pia hata kama ukifikisha idadi hiyo pia inategemea na video zako kama zinafaa kwa matangazo ama laah.

 2. naomba boss unisaidie kidogo mm nimefungua YouTube channel yangu mwezi wa Tano huu lakini nimeweka videos kama watu wanaangalia basi niwawili sasa sijui tatizo ninini ?wakati wenzangu wakiweka video Leo kesho watu hata laki 5 kashafikisha kwa video moja