in

Facebook Yaleta Sehemu Mpya ya Facebook Stories

Sasa kutana na Stories kwenye programu za Facebook za Android na iOS

Facebook Yaleta Sehemu Mpya ya Facebook Stories

Mapema leo kampuni ya facebook imeanza kuleta toleo jipya la facebook lenye sehemu ya Facebook Stories kama ilivyo kwenye programu za Instagram pamoja na Snapchat. Sehemu hiyo mpya itakuwa kwenye programu ya Facebook ya mifumo yote yani Android pamoja na iOS.

Sehemu hiyo haina haja ya kutafuta sana kwani inapatikana juu kabisa kama ilivyo kwenye programu ya mtandao wa Instagram. Kwa sasa kama bado huja-update programu yako anza sasa kwani toleo jipya lenye sehemu hiyo limetolewa leo kote duniani.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Matumizi ya Facebook Stories yako sawa kabisa na matumizi ya Snapchat stories hivyo huna aja ya kuwa na wasiwasi kuhusu jinsi ya kutumia. Kama bado ujapata toleo jipya la Facebook lenye sehemu hii usiwe na wasiwasi angalia update kupitia programu zako za Android kwenye Play Store na iOS kwenye App Store kama pia bado ujaona update hizo usijali subiria ndani ya kama siku moja kwani update zinachukua muda kidogo kufika kwa watumiaji wote wa facebook duniani.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

Jinsi ya Kusajili Biashara Kupitia Google My Business (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.