in

Hivi Ndivyo Ilivyo Rahisi Ku-Hack Simu ya Raisi Donald Trump

Hivi ndivyo ilivyo rahisi kuhack simu ya raisi wa marekani Donald Trump

Donald Trump

Raisi wa marekani Donald Trump bado anatumia simu yake ya Android, pamoja na nguvu na ushawishi uliotumika kumkataza raisi huyo kutumia simu yake lakini bado anaendelea kutumia simu hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya The verge Donald Trump bado anatumia simu ya aina ya Samsung Galaxy S3 kutoa mawazo yake mbalimbali kwenye mtandao wa Twitter. Pamoja na marekani kuwa moja kati ya nchi zinazojua kutunza siri zake, huenda wakati huu nchi hiyo ikashindwa kufanya hivyo. Katika video iliyotengenezwa na mtandao wa The Verge ilikua ikionyesha jinsi ilivyo rahisi ku-hack simu ya raisi huyo na kuigeuza kuwa kinasa sauti ambapo hacker uweza kubadilisha na kutumia simu hiyo kama kifaa cha kusikila mazungumzo ya raisi Donald Trump.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Video hiyo ya mfano ilikua ikionyesha jinsi mfanyakazi wa kampuni ya The verge alivyo mtumia mtaalamu kuhack simu ya mfanyakazi mwenzake aina ya Samsung Galaxy S6 na kuibadilisha kuwa kama kifaa cha kusikiliza yote ailiyokuwa anaongea.

Mpaka sasa repoti zinaendelea kusema kuwa bado Donald Trump anatumia simu yake ya Samsung Galaxy S3 ambayo haina ulizi wa kutosha, raisi huyo alionekana na simu yake hiyo toka mwaka 2015 na inasemekana mpaka sasa bado anatumia simu hiyo na amegoma kabisa kubadilisha simu hiyo kwa mujibu wa tovuti ya The New York Times.

Kwa Habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App ya Tanzania Tech kupitia Play Store, pia unaweza kujiunga na channel yetu Youtube ili kupata habari za teknolojia na maujanja mbalimali kwa njia ya Video.

Infinix Yashinda Tuzo za Design Kimataifa (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.