in

Hii Ndio Simu Mpya ya LG G6 Inayo Tarajiwa Kutoka February 26

Simu mpya ya LG G6 inayotarajiwa kutoka tarehe 26 february mwaka huu

LG G61

Hivi karibuni kampuni ya Korea ya LG imethibitisha kua iko tayari kutoa toleo lake jipya la simu mpya ya LG G6, Simu hiyo inayotarajiwa kutoka mwezi wa pil (February) ni moja kati ya simu zinazotarajiwa kuzinduliwa kwenye mkutano wa maonyesho wa CES wa Mwaka 2017.

Simu hiyo ya LG G6 inatarajiwa kuja na sifa za kioo kikubwa cha inch 5.7 pamoja na simu hiyo kusemekana kuwa na kioo kikubwa, simu hiyo pia inatarajiwa kuja na uwezekano wa kuwa na asilimia 90 ya kioo kitupu kama picha inavyoonyesha hapo chini.

Simu hiyo pia inasemekana kuja na maboresho mapya na bora zaidi kuliko yale ya kwenye toleo lililo pita, Kumbuka usikose kuangalia uzinduzi huo live kupitia hapa hapa Tanzania Tech.

Kwa Habari zaidi za Teknolojia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech kupitia Play Store au unaweza kujiunga na Youtube Channel yetu ya Tanzania Tech ili kujifunza zaidi teknolojia kwa njia ya Video.

Kampuni ya Nokia Kubadilisha Logo Yake ya "NOKIA"

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.