in

Laptop Bora Kwenye Mkutano wa CES wa Mwaka 2017

Angalia laptop hizi bora zilizoonekana kwenye mkutano wa CES 2017

laptop Bora CES 2017

Leo ni mfululizo wa siku ya tatu ya maonyesho makubwa ya teknolojia duniani CES ambayo yanafanyika huko Las Vegas, Nevada, kwa siku ya leo tunakuletea laptop bora ambazo zimeonekana kwenye mkutano huo kuanzia mkutano huo ulipo anza hapo juzi. Laptop hizi ni moja kati ya laptop ambazo pengine ungependa kununua ndani ya mwaka huu wa 2017.

Samsung Notebook 9

Samsung Notebook 9 ni moja kati ya laptop bora sana kwenye mkutano wa CES wa Mwaka huu wa 2017, laptop hii imetengenezwa kwa muundo bora pamoja na teknolojia ya kisasa. Kuhusu sifa laptop hii kwa ufupi laptop hii imetoka pamoja na laptop nyingine nne hivyo habari zaidi pamoja na sifa za laptop hii tembele tovuti ya Samsung.

Samsung Chromebook Plus

Laptop hii ya Samsung Chromebook Plus tulipata kuiona jana kwenye list ya bidhaa bora za kwenye mkutano wa CES leo pia laptop hii imeweza kushika namba kwenye list hii ya laptop bora kwenye mkutano huo wa CES wa mwaka 2017.

Nunua Laptop Bora Kwa Kuangalia Jina la Processor

 Asus ZenBook 3 Deluxe UX490

Hii ni laptop kutoka kampuni ya Asus laptop hii ni moja kati ya laptop bora zilizotangazwa na kampuni hiyo kwenye mkutano huo wa CES 2017, Laptop hii ina processor ya Intel® Core™ i7 processor pamoja na ram ya GB 16, Vile vile laptop hii imetengenezwa kwa teknolojia Gorilla Glass 5 ambayo ni maalum kwa kulinda kioo cha laptop hiyo. Kuhusu sifa zaidi za laptop hii unaweza kupitia tovuti ya Asus.

ASUS Transformer Pro T304

Kwa mara nyingine kampuni ya Asus imeingiza laptop nyingine ya ASUS Transformer Pro T304 laptop hii ni moja kati ya laptop ambazo ni 2 in 1, laptop hii inauwezo wa kuwa laptop na kuwa desktop zote zikiwa na uwezo na teknolojia ya hali ya juu.

HP EliteBook x360 G2

Kwa mara nyingine tena kampuni ya HP imeleta laptop yake nyingine ya HP EliteBook x360 G2 laptop hii ni moja kati ya laptop bora kutoka kampuni ya HP na inasemekana kuwa ni laptop bora kuliko nyingine.

Laptop za Mwaka 2021 Ambazo ni Bora Kwa Matumizi 2023

Razer Project Valerie

Kama wewe ni mpenzi wa Game basi laptop hii mpya kutoka kampuni ya Razer ni laptop bora sana kwako, Laptop hii imetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa ikiwa na vioo vitatu ambavyo vitakuwezesha kucheza game zako kwa urahisi uku ukifurahia manthari kwa vioo vitatu vya laptop hiyo. Kwa habari zaidi kuhusu laptop hii unaweza kutembelea tovuti ya kampuni hiyo ya Razer.

Dell XPS 15 na Dell 2 in 1

Dell nayo haikua nyuma na ilifanikiwa kutoa laptop mbalimbali kakini moja kati ya laptop bora ni Dell XPS 15 na dell 2 in 1 zote zikiwa na processor mpya na bora za mwaka 2017.

Kujua zaidi kuhusu sifa za undani pamoja na bei za laptop hizi endelea kutembelea Tanzania tech kila siku na tutakupa habari mpya za teknolojia kila siku. Pia kupata habari za teknolojia za haraka unaweza kudownload App ya Tanzania Tech kupitia Play Store.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment