in

Sasa Unaweza Kutumia Window 98 Kwenye Saa ya Apple

Saa ya Apple

Ikiwa ni miaka 21 toka kampuni ya microsoft kutengeneza window 98 sasa unaweza kuhifadhi (install) window hiyo kwenye saa ya Apple (Apple Watch), mmoja wa waandishi wakubwa wa habari za teknolojia duniani amesikika akisema “kwa sasa teknolojia iko mbali sana ukilinganisha na miaka 21 iliyopita kwani kwa kuhifadhi Window 98 kwenye saa hii unaweza kufanya mambo mengi ambayo tulikua tukiyafanya wakati ule kwenye kompyuta, hichi ni kitu cha kufurahisha na cha-kushangaza jinsi teknolojia inavyo badilika kila siku”.

Hata hivyo kwa kuhifadhi window 98 kwenye saa hiyo ya Apple utaweza kucheza game mbalimbali za window 98 pamoja na kusikiliza muziki na mambo mengine mengi, hata hivyo mtaalamu wa maswala haya ya teknolojia aliyewezesha ujanja huu kufanikiwa Mr. Nick Lee kutoka kampuni ya Tendigi ambayo inajihusisha na maswala ya teknolojia nchini marekani alisema kuwa “ili kufanya saa yako ya Apple iweze kusoma window 98 inakuitaji uwe na subira  pamoja na utaalamu kiasi hata hivyo sio rahisi kama inavyofikiriwa kwani ili ku-install window hiyo kwenye saa hii inakubidi utumie masaa zaidi ya saba kwani window hiyo inatumia zaidi ya lisaa limoja kuwaka (ku-boot) kwenye saa hiyo ya Apple hivyo inahitaji sana uvumilivu”.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Pia mtaalamu huyo aliandika kwenye blog yake hatua kwa hatu namna ya kuhifadhi window hiyo kwenye saa hiyo ya Apple, hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa kinara huyo wa teknolojia nchini marekani kucheza na vifaa mbalimbali vya teknolojia awali alitangaza kuwa ameweza kuhifadhi (ku-install) Mac OS kwenye saa ya Apple.

Cheki video ya ujanja huo hapo juu.

Jinsi ya Kutengeneza Akaunti ya Threads Hatua kwa Hatua

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments